Tanzania yapewa heshima ya kipekee uchaguzi wa Kenya

NA DIRAMAKINI

SIKU chache, baada ya Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Jakaya Kikwete kupewa heshima ya kuongoza tume ya waangalizi wa uchaguzi nchini Kenya kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Mtanzania mwingine ambaye ni Muhubiri na Mwinjilisti wa Kimataifa, Bw.Alphonce Temba leo Agosti 5,2022 ni miongoni mwa wana jopo watakaoshiriki maombezi maalumu ya kumuomba Mungu na kumshukuru katika mbio za Urais nchini humo.

Jopo hilo ambalo halihusiani na tume ambayo inaongozwa na Dkt.Kikwete ambayo ni timu ya watu 52 kutoka taasisi muhimu za serikali na huru za mataifa wanachama pamoja na mashirika ya kiraia inaamini kuwa, uangalizi wa kikanda ni muhimu ili kuzidisha uaminifu wa uchaguzi, kuongeza nguvu ya makundi ya waangalizi wa ndani, na kuimarisha imani ya umma katika mchakato mzima wa uchaguzi.

Kwa nini Temba?

Mwinjilisti Temba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Penuel Radio ilyopo Marangu mtoni mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania kwa miaka mingi amekuwa akitumia kipawa na karama aliyopewa na Mungu ya kusema na kufafanua kile ambacho Mungu amemsemesha kwa ajili ya mataifa mbalimbali duniani.
Karama hiyo, imekuwa ikimpa heshima kubwa mbele ya wakuu wa nchi na hata mataifa mbalimbali ikiwemo ndani ya Tanzania, barani Afrika na hata duniani kwa ujumla.

Mwaka jana, Mwinjilisti Temba alitabiri juu ya ushindi wa Chama cha United Party for National Development (UPND) kilichomwingiza madarakani Rais Hakainde Hichilema wa Zambia.Ambapo pia alishiriki katika hafla ya kuapishwa kwa Hichilema iliyofanyika Agosti 24,2021 jijini Lusaka nchini Zambia.

Mwinjilisti Temba alipokelewa Zambia na Mwenyekiti wa Taifa wa chama tawala, Stephen Katuka ambapo kwa sasa ameteuliwa kuwa Balozi wa Zambia nchini Namibia.

Pia alimwahidi kumwalika tena mara ya tatu kumuombea rais maombi maalumu Ikulu ya Zambia ambapo amewahi kufanya maombi mara mbili mwaka 2004 wakati wa Rais Mwanawasa na mwaka 2013 wakati wa Rais Michael Sata wote sasa ni marehemu.

Alivyoalikwa mara ya pili, Mwinjilisti Temba ilikuwa ngumu kukutanishwa na rais kwa sahabu alikuwa akielekea nje ya nchi kwa ziara ya kikazi kwa mara ya kwanza baada ya kuapishwa kuwa rais wa Zambia,ikumbukwe kutokana na kuonya nchi ya Zambia kuwa ni lazima kufanya maombi kabla rais kuingia Ikulu, lasivyo yatatokea mambo mengi mabaya kiuchumi na kiafya, hata hivyo rais tangu hasikie habari hiyo hajaweza kuhamia Ikulu, yupo kwake hadi leo jambo ambalo si la kawaida.

Aidha,moja ya tabiri kubwa aliyowahi kutitoa ni pamoja ya kumuonya aliyekuwa rais wa Zambia Levi's Mwanawasa mwaka 2006 kuwa atashinda uchaguzi mkuu Zambia mwaka 2006 lakini hatokaa sana madarakani jingine ni kumwombea aliyekuwa Rais wa Zambia,Frederick Jacob Titus Chiluba kushinda kesi na akashinda pamoja na kumwandikia hayati rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa alikuwa akiona ana maisha kama ya Mwanawasa kama hatoombewa na yeye.

Pia amewatabiria viongozi wengi wakashinda uchaguzi akiwemo aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Waziri wa Mambo ya Nje mwaka 2004 na Hayati Michael Sata aliyekuwa rais wa Zambia na Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na wengine wengi.

Akiwa jijini Nairobi, Mwinjilisti Temba amesema ngome ya Raila Odinga na makamu wake, Martha Karua (Iron Lady) inakabiliwa na vikwazo viwili ambavyo vilionekana vinakwenda kumkwamisha Raila kuchaguliwa kuwa mrithi wa Rais wa sasa Uhuru Kenyatta.

Mwinjilisti Temba baada ya kupokelewa na Katibu wa Mheshimiwa Raila, Andrew Mondoh katika ofisi zao zilizoko Capital Hill Square, 4th Floor Upperthil, Nairobi alifanya mkutano wa nusu saa ukiwahusisha Mheshimiwa Raila kwa njia ya mtandao kwa kuwa alikuwa nje ya Nairobi kwa kampeni na kuyaeleza yale Mungu anayomuonesha na hivyo vikwazo ambavyo tayari ameviwasilisha kwa wahusika.

Mwinjilisti Temba alieleza vikwazo hivyo ambavyo vilionekana kuwa na mashiko na ndịpo majadiliano upande wa pili yalipotoa maelekezo kuwa,awepo katika jopo la watumishi wa Mungu ambao watafanya maombezi maalumu ya kumuomba Mungu na kumshukuru katika mbio za Urais.

Ni mbio, ambazo mwaka huu zimekuwa na uzito mkubwa kutokana na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kuamua kuacha kumuunga mkono makamu wake, William Ruto na kumuunga mkono mpinzani wake, Raila Odinga.

Wakenya wengi wanaamini Rais Uhuru aliamua kumuunga mkono akiwa anaiga moyo wa Hayati rais wa Pili wa Kenya Arap Moi ambaye aliachiwa jukumu la kumlea na marehemu Mzee Kenyatta.

Hata hivyo, historia ya Kenya inaonesha kuwa kulikuwa na uswahiba mkubwa kati ya mzee Kenyatta, rais wa kwanza na baba mzazi wa Raila Mzee Odinga ambaye aliwahi kuwa makamu wa Rais kipindi hicho, hata hivyo kuna kipindi mzee Kenyatta aliwekwa ndani na wakoloni wakampatia nchi Odinga kuwa Rais, hata hivyo aligoma na ndiye aliyesababisha mzee Kenyatta kuachiwa na kuendelea kuwa Rais wa Kenya.

Hivyo, kuna imani kubwa kuwa, machifu walikuwa wakimsonga muda mrefu Kenyatta kuangalia fadhila kutokana na historia ya wazazi wao. 

Vilevile vile, Mwinjilisti Temba alibainisha kuwa, iwapo William Ruto atashinda Urais wa Kenya, uongozi wake utapitia katika tanuru la moto.

"Mheshimiwa Ruto anaweza kushinda Urais, lakini ushindi wake unaweza kuwa wa furaha kipindi cha awali, kadri siku zitakaposonga mbele uongozi wake utageuka kuwa tanuru la moto, ninaona linaweza kuibuka vuguvugu la vijana ambao watakuwa hawakubaliani na namna ambavyo hali ya kiuchumi itakavyokuwa,"alisisitiza Mwinjilisti Temba.

DIRAMAKINI ilivyokuwa ikimuhoji, Mwinjilisti Temba kuhusu kupata mwaliko huo nyeti toka kwa viongozi wa kisiasa nje ya nchi ikizingatiwa nchi ya Kenya imekuwa na changamoto kadhaa hasa kipindi hiki cha uchaguzi, amesema, kila jambo linakuja na kutimia kwa kusudi la Mungu.

Hili linajidhihirisha wazi ni neema ya wafalme kama ya Eliya na Samwelị iliyoko ndani yake ambayo inafanya kazi kutokana na taarifa hizo za kinabii, kutokana na joto la uchaguzi DIRAMAKINI litazieleza baada ya uchaguzi kupita.

Ikumbukwa kuwa, mwaka jana Mwinjilisti Temba akitokea Zambia katika uchaguzi alifika Ikulu ya Botswana na kukutana na Waziri anayehusika na Masuala ya Rais, Utumishi na Utawala wa Umma, Mheshimiwa Kabo Neale Sechele Morwaeng.

Akizungumza baada ya kuwasili Botswana, Mwinjilisti Temba alisema, ameendelea kuitikia wito wa Mungu wa kwenda kutamka neno la uponyaji na ushindi kwa mataifa mbalimbali Kusini mwa Afrika.

Maombi yanaweza kuwa silaa tosha. Ikizingatiwa kuwa, Botswana walifungia watu ndani na kila wiki waligawa chakula nyumba zote nchi nzima na nusu ya wananchi walikuwa wamechanjwa, lakini ilikuwa na vifo vingi ikifuatiwa na India kulingana na takwimu za mara kwa mara wakati huo.

"Ninamshukuru Mungu, baada ya kuingia Ikulu na kupokelewa na Waziri Ofisi ya Rais, Mheshimiwa Kabo baada ya maongezi pamoja na washauri wa rais wakakubaliana nami kuwa sasa Botswana kwa mara ya kwanza Serikali iitishe maombi ya mwezi mzima kumlilia Mungu,"alisema ambapo baada ya maombi Serikali iliwaachia huru wananchi wakaendelea na majukumu yao.
 
Pia Mwinjilisti Temba katika uchaguzi wa Malawi alitabiri, ambapo mgombea wa upinzani Askofụ Lazarus McCarthy Chakwera alikuwa amekimbilia mahakamani,licha ya Rais wa Malawi,Arthur Peter Mutharika Petre ambaye alikuwa ameshaunda serikali ndani ya miezi nane na Mwinjilisti Temba alitabiri Rais Mutharika kushindwa mahakamani na uchaguzi ungerudiwa na Chakwera angeibuka mshindi na yote yakatokea kama neno la mtumishi wa Mungu alivyonena.

Wakati huo huo, Muhubiri na Mwinjilisti Temba alikuwa mtumishi wa kwanza kupeleka ujumbe wa kinabii katika Gereza la Ukonga lililopo jijini Ilala, Dar es Salaam na kumtabiria, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe kuwa, Mungu angefanya jambo juu yake. Aidha, siku chache baadae aliachiwa huru kutoka gerezani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news