TCRA yakabidhi vifaa vya TEHAMA kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka

NA MWANDISHI MAALUM

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekabidhi vifaa vya TEHAMA kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa lengo la kuongeza ufanisi wa kazi zikiwemo kompyuta Mpakato 11, kompyuta za mezani 5, Mashine ya kunakilia 1 na Mashine ya kuchapia (Printa )1.
Akikabidhi vifaa hivyo katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka leo Jijini Dodoma Mkurugenzi wa Sheria kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Modestus Ndunguru ameitaka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuvitumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili vikalete tija na mchango mkubwa kwa Watanzania.

“Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inafarijika sana inapotoa vifaa hivi kwa Taasisi lakini faraja ni kubwa zaidi hicho kinachotolewa kinapata Thamani kubwa kutokana na mchango wa mtumiaji.Ofisi ya Mashtaka ndiyo itakayoleta thamani ya vifaa hivyo kwa Jamii, nendeni kavitumieni vifaa hivi kwa huduma nzuri ili mafao yafike kwa jamii." Amesema Modestus Ndunguru.

Aidha, Nduguru Amesema katika Kompyuta Mpakato 11 watakabidhi Kompyuta Mpakato 5 na kubakia Kompyuta Mpakato 6 ambazo zitakabidhiwa muda mfupi ujao ambapo amesema wataendelea kutoa vifaa vya TEHAMA kwa Taasisi mbalimbali nchini ili kuongeza ufanisi na urahisishaji wa kazi.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Joseph Pande ameihakikishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwamba vifaa hivyo vitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na vitatunzwa kwa kila namna ili vikalete matokeo chanya katika kuwahudumia Watanzania.

“Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kama zilivyo ofisi zingine za haki jinai zina mahitaji makubwa ya vifaa vya TEHAMA. Mikoa ya Kimashtaka Tanzania ipo 30 na inahitaji vifaa vya TEHAMA, ninaahidi kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwamba vifaa hivi vitaenda kutumika vizuri lakini pia kutokana na uhitaji mkubwa wa vifaa hivi kesho vinaenda kutumika na havitokaa stoo kwa sababu mahitaji yake ni makubwa” amesema Bw.Joseph Pande.

Ikumbukwe kuwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeanzishwa kama Ofisi huru ya Umma kupitia Tangazo la Serikali na 49 la Mwaka 2018 la tarehe 13 February 2018 la kuanzisha Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa ajili ya kutekeleza Mamlaka ya kikatiba aliyopewa Mkurugenzi wa Mashtaka ya kusimamia haki jinai kwa Mujibu wa Ibara ya 59B ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news