NA MWANDISHI WETU
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wamefika Salasala jijini Dar es salaam nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema ili kutoa pole.

Sambamba na kuifariji familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia
kifo cha kiongozi huyo aliyefariki tarehe 21 Agosti 2022 katika
Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es salaam.
Akiwa nyumbani hapo, Makamu wa Rais amewapa pole wana familia na kuwaomba kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiongoza sala ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema walipofika msibani nyumbani kwa marehemu Mrema eneo la Salasala jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais amesema, marehemu Mrema alikuwa ni kiongozi mkweli na mzalendo kwa taifa ambapo wakati wote alitetea maslahi ya nchi.
Amesema, taifa limepoteza kiongozi aliyetumikia vizuri nafasi zote alizowahi kuongoza katika uhai wake.