NA WANGWE JR
UHURU wa kila mtu kutoa matokeo ya uchaguzi umedhihirisha aibu na fedheha kwa wapenda demokrasia na wachambuzi wa masuala ya siasa barani Afrika na Duniani kote.
Tume ya Uchaguzi ndio inapaswa kutoa takwimu ili kuepusha mikanganyiko isiyo na tija.
Upande mwingine mshindi wa Ubunge wa Jimbo la Kimilili, Bwana Didmus Barasa amedaiwa kumuua msaidizi wa aliyekuwa mshindani wake katika kinyang'anyiro cha Ubunge wa jimbo hilo.
Hii ndio maana ya familia ya Kambale yaani kila mmoja ana ndevu, hakuna kuheshimu sheria.
Jioni hii kituo cha kuhesabia kura cha Kirinyaga kimevamiwa na wafuasi wa wanasiasa Anne Waigiru na mwenzie Wangui Ngirici.
Yanayoendelea ni mfano mbaya ambao unapaswa kuchukuliwa kama somo na nchi nyingine ili kuepusha uhuni kutamalaki katika mawanda ya Demokrasia hapa Afrika.
Mchakato wa Uchaguzi nchini Kenya ni mfano mbaya usiopaswa kuigwa hata punje, ni kama Familia ya Kambale kila mmoja anafanya anavyojisikia.