NA DIRAMAKINI
"Nilikuwa nasubiri kwa hamu kuhesabiwa, sikuwa nashinda nyumbani ila niliacha taarifa zote sasa kila nikiuliza wamekuja hola. Bahati nzuri leo sijatoka, asubuhi mapema karani akawasili nimesabiwa sasa hivi nina amani sana,"amesema mmoja wa wakazi wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Wakati huo huo,Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Mheshimiwa Jokate Mwegelo ametoa wito kwa makarani kuhakikisha wanafanya kazi hiyo kwa kasi na weledi mkubwa ili Serikali ipate takwimu na taarifa sahihi.
Ametoa wito huo leo baada ya kumaliza kushiriki zoezi la usafi wa mazingira katika Kata ya Chamanzi iliyopo wilayani humo,“Tumehamasisha wananchi wajiandae kuhesabiwa na tumepata ushirikiano mkubwa, niwaombe makarani jitahidini kazi hii ikamilike kama ilivyopangwa, nataka wilaya yetu iibuke kidedea kwenye sensa.
“Kata ya Chamazi ina watu wengi na ndiyo maana jana tuliongeza makarani huku, sasa niwaombe makarani hebu malizieni hili kwa ufanisi, sitaki ifike siku ya mwisho awepo mtu ambaye hajahesabiwa,"ameelekeza Mheshimiwa DC Jokate.
Wadau wengine wanasemaje? Endelea hapa chini;