NA MWANDISHI WETU
VIJANA saba ambao ni wataalam wa afya pamoja na mwanasheria mmoja kutoka katika Jiji la Dar es Salaam wamejiajiri kwa kufungua zahanati kupitia mkopo wa halmashauri.
Zahanati hiyo wameifungua Kipunguni kwa Mkolemba Halmashauri ya Wilaya ya Ilala baada ya kupatiwa shilingi milioni 110 ambazo ni sehemu ya mkopo utokanao na ukusanyaji wa mapato ya asilimia 10 ya halmashauri.
Miongoni mwa vijana hao kati yao wamo madaktari wawili, mfamasia mmoja, wataalam wa maabara wawili, manesi wawili na mwanasheria mmoja ambapo jana zahanati yao imezinduliwa rasmi na Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mhe. Jerry Silaa.
