NA GODFREY NNKO
LEO dola ya Zimbabwe (ZWD) inanunuliwa kwa shilingi 0.43 na kuuzwa kwa shilingi 0.44 huku Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2350.75 na kuuzwa kwa shilingi 2375.18.
Aidha,Paundi ya Uingereza (GBP) inanunuliwa kwa shilingi 2779.11 na kuuzwa kwa shilingi 2807.83 huku Yuan ya China (CNY) ikinunuliwa kwa shilingi 339.71 na kuuzwa kwa shilingi 343.02.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Agosti 11, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Dirham ya Umoja wa Falme za Kiarabu (AED) inanunuliwa kwa shilingi 624.39 na kuuzwa kwa shilingi 630.49 huku Schilling ya Australia (ATS) ikinunuliwa kwa shilingi 147.15 na kuuzwa kwa shilingi 148.46.
Krona ya Sweden (SEK) inanunuliwa kwa shilingi 226.40 na kuuzwa kwa shilingi 224.47 huku Randi ya Afrika Kusini (ZAR) ikinunuliwa kwa shilingi 139.34 na kuuzwa kwa shilingi 140.59.
Shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.57 na kuuzwa kwa shilingi 0.59 huku Franka ya Burundi (BIF) ikinunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21.
Kwacha ya Malawi (MWK) inanunuliwa kwa shilingi 2.08 na kuuzwa kwa shilingi 2.21 huku Rupia ya Pakistan (PKR) ikinunuliwa kwa shilingi 9.83 na kuuzwa kwa shilingi 10.44.
Rupia ya India (INR) inanunuliwa kwa shilingi 28.86 na kuuzwa kwa shilingi 29.14 huku Shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.24 na kuuzwa kwa shilingi 19.41.
Franka ya Rwanda (RWF) inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.25 huku Yen ya Japan (JPY) ikinunuliwa kwa shilingi 17.01 na kuuzwa kwa shilingi 17.18.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
Biashara na Masoko
Fedha na Uchumi
Fedha za Kigeni
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania