Waziri Bashungwa asema yasiyofahamika kuhusu Sensa

NA OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amesema OR-TAMISEMI ni mdau mkubwa wa takwimu zitakazokusanywa kwenye Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23,2022 ili kuimarisha upelekeaji wa huduma kwa wananchi.

Waziri Bashungwa ameyasema hayo leo Agosti 16, 2022 wakati wa mahojiano katika kipindi cha Powerbreakfast cha Clouds Fm jijini Dar es Salaam.

Amesema, katika upangaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo hususani upelekaji wa huduma za kijamii na kiuchumi karibu na wananchi zinahitaji takwimu sahihi ya idadi ya watu ili huduma hizo ziweze kwenda kwa uwiano na idadi ya watu.

"Huduma hizo ni pamoja na ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya kwa maana ya hospitali, vituo vya afya na zahanati, huduma za elimu yaani shule, madarasa, ujenzi wa maabara, mabweni, maabara, miundombinu ya maji pamoja na kufanya msawazo wa watumishi kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa.

"Kwa mfano OR-TAMISEMI inatekeza upatikanaji wa huduma za afya bure kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano sasa kama hatuna takwimu sahihi hatuwezi kutekeleza jukumu hili ipasavyo na kwa hivyo kuna baadhi ya watoto hawatapata huduma hii kwa sababu tu hawakuhesabiwa na kwenye takwimu zetu hayupo hivyo tunashindwa kumu-accomodate (kumjumuisha),”amesema Mheshimiwa Bashungwa.

Amesema, kwa upangaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo katika Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa (MSM) takwimu zilizokuwa zikitumika ni takwimu ambazo zinapatikana baada ya kufanya makadirio kwa kutumia Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 kama “base year”.

” Tunatambua kuwa kuna mabadiliko makubwa yametokea katika kipindi cha miaka 10 tangu sensa ya mwisho ifanyike yaani mwaka 2012 hadi 2022, hivyo Sensa hii itakuwa ni msingi wa kupata takwimu halisi zitakazohakisi mabadiliko hayo, kuwezesha kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo na kufanya maamuzi sahihi kwa maendeleo ya wananchi wetu kwa kipindi cha miaka 10 au zaidi ijayo,”amesema.

Mhe. Bashungwa aliwaka wakuu wa mikoa, makatibu tawala,wakuu wa wilaya,makatibu tawala wilaya na wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kutotoka kwenye maeneo yao ya kazi mpaka Sensa ya Watu na Makazi litakapokamilika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news