Waziri Prof.Mkenda afunguka kuhusu ada, michango shuleni

MA GODFREY NNKO

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema, tayari Kamishna wa Elimu nchini anapitia muongozo wa waraka wa michango shuleni ili kuja na njia bora ambayo itaondoa michango ya shinikizo badala yake iwe ya hiari pale inapolazimika.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe.Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari juu ya Mwelekeo wa Wizara, Vipaumbele na Maeneo ya Kimkakati katika Utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2022/23.

"Mnafahamu kwamba Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo kwamba elimu bila malipo iende form five na six, kwa hiyo mpaka sasa hivi elimu bila ada Tanzania ni kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha sita, kwa namna hiyo kwa kweli tunakuwa tunatekeleza commitment yetu ya sustainable goal ya kutoa free education mpaka kidato cha sita. Na hapa niongezee mambo mawili.

"Tunapitia, na Kamishna wa Elimu tumemwambia apitie muongozo na waraka wa michango shuleni kupunguza, kwa sababu sasa tamaa inakuja, Rais ametuambia tuondoe ada, halafu tunaona michango inapitia katika nyanja nyingine kwa hiyo tunataka hiyo michango mingine yote lazima iwe ni ya hiari.

"Sasa of course inapokuwa ni ya hiari bado kunakuwa na shinikizo fulani kwa wale ambao hawajachanga kwa hiyo waraka unapitiwa, tutautangaza lakini wakati huo huo tunahimiza shule, halmashauri zihakikishe zinapunguza michango hii ambayo inaonekana inakinzana na mwelekeo wa Serikali kwa kuhakikisha kwamba tunapunguza gharama za elimu hiyo, hiyo ni namba moja.

Jambo la Pili

"Namba mbili, bado tunahimiza watu waliosoma katika shule mbalimbali whether una mtoto pale au hauna, kwenda kusaidia shule kuwekeza, juzi pale Rombo nimepokea watalii kutoka Israel, ni walimu, mameneja wa shule wamestaafu wamekuja kusaidia kujenga madarasa, sisi ambao tumesoma...mimi nimesoma Pugu kwa mfano sisi tunaweza kuchanga tukaenda kusaidia Serikali kuboresha elimu hasa shule za msingi ambapo tunataka michango hiyo ya hiari inaweza ikaendelea, lakini hakuna mwanafunzi kurudishwa nyumbani kwa sababu ya michango.

Chakula shuleni

"Na kuna suala lingine la muhimu watoto kula shuleni, wazazi wanapokutana wakakubaliana kwamba tuchangie fedha kwa ajili ya watoto kula shule hilo ni jambo jema sana, sasa hilo wazazi wanaweza wakali-manage (kumudu) wenyewe, bado michango ya hiari haiwezi kuwa ni kigezo cha kurudisha mtoto nyumbani.

"Wazazi wakikubalina kwa pamoja wakahimizana watoto wanaweza wakala chakula shuleni. Hilo ni jambo zuri, lakini kama ilivyo, kwa sasa Serikali msimamo wake hakuna mtoto atarudishwa nyumbani kwa sababu ya kutokuchangia chochote.

"Narudia tena, hakuna ada na maelekezo ya Mheshimiwa Rais tuhakikishe tunayazingatia, utitiri wa michango unaongezeka wakati ada imeondolewa, lakini tutalisimamia Kamishna wa Elimu analifanyia kazi na atatoa waraka siku za hivi karibuni,"amefafanua Prof.Mkenda.

Uwekezaji

"Pia nazungumzia kuhusu upatikanaji wa elimu, vile vile mnafahamu kwamba Serikali imewekeza sana katika elimu maalum kwa wale ambao wana changamoto mbalimbali na juzi hapa tumegawa kompyuta za kuwasaidia, sasa hivi tunachapisha vitabu vya maandishi maalum wa wenzetu ambao hawawezi kuona wanaweza wakasoma kwa vidole, kwa mara ya kwanza tumeshachapisha vitabu kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha sita ili kuhakikisha hawa wanapata elimu bora.

"Tumeweza kugawa na printers ambazo zinaweza kuprint,na kuweka utaratibu ambao unaweza kuwasaidia kufanya mitihani kwanza tuna-translate ( tafsiri) maandishi ambayo ni maalum kwenye maandishi ambayo ni kawaida kwa ajili ya walimu kusahihisha na serikali imejenga shule mpya kwa ajili ya mahitaji maalum.

"Shule moja ipo Arusha juzi Naibu Waziri wetu wa Elimu Sayansi na Teknolojia alikwenda kuizindua. Na mimi nitakwenda Mtwara kwenda kuzindua shule nyingine, lakini tuna mfumo wa kutoa elimu mchangangiko kwa kuchanganya wanafunzi ili watu wasijione wamejitenga.

"Uhuru Mchanganyiko kwa mfano alivyokuja Waziri wa Elimu Msingi wa Afrika Kusini alivyokwenda kutembelea pale alifurahi sana, alisema na wao wana cha kujifunza, kwa hiyo, timu yao iliongozwa na Naibu Katibu Mkuu ambao nilikutana nao na wenyewe walienda pale walisema wanataka kujifunza jinsi Tanzania inavyoweza kuwachanganya wanafunzi wenye mahitaji maalum na wale ambao hawana mahitaji maalum na wanasoma kwa pamoja ili kila mmoja ajisikie vizuri.

Msisitizo

"Hayo ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais wetu mtakumbuka yeye mwenyewe alishatembelea Benjamini Mkapa shule pale, alitembelea kwa sababu wanafunzi walimualika, alikuwa na msukumo kwa sababu aliona wale walimwinbia Happy Birthday akaona wana changamoto alisema nakuja kuitembelea shule na alitoa maelekezo vitu vya kufanya kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa elimu kwa watu wenye mahitaji maalum.

"Na muongozo tumeutoa tunapotaka kujenga shule sasa hivi tufanye nini hata wenye changamoto za kutembea, kuona, kusikia wanaweza wakapata elimu.

"Na la mwisho ninalotaka kulisema kuhusu upatikanaji wa elimu ni hatua alizozichukua Mheshimiwa Rais Samia kwa kusema kwamba, jitahidini rudisheni watoto walioacha shule warudi wakamalize shule kwa sababu mbalimbali. Hata waliopata ujauzito, lakini sio hao hata ukiangalia shule za msingi wanaoacha shule wengi ni wavulana na si tu wanawake kwa hiyo jitihada hizo zinafanyika na tumeona mwitikio unaenda vizuri.

Maelekezo

"Na maelekezo ya Rais wetu ni kwamba watoto wenye familia zenye uwezo kwa mfano akapata ujauzito akajifungua. Wazazi wanamlipia private anamaliza shule, anaweza akatimiza ndoto yake, watoto wenye familia ambazo zisizojiweza kwa kuwaondoa mashuleni moja kwa moja inamaana unazima ile ndoto ya kuendelea kusoma.

"Kwa hiyo tunaendelea nalo, tulienda juzi kwenye shule tulitembelea na Makamu wa Benki ya Dunia tuliongea na wanafunzi ni katika hatua ambazo zinachukuliwa na Serikali katika upatikanaji wa elimu.

"Kwa hiyo nilianza kwa kusema kwenye elimu kuna mambo mawili, kwa maana ya ubora wa elimu na upatikanaji wa elimu sasa hizi ni hatua za upatikanaji wa elimu to increase axcess to education.

"Kwenye ubora nimezungunzia kuwa kuelewa kile ambacho kinatolewa mashuleni, lakini kuhakikisha kile ambacho kinatolewa kina hakisi kweli mahitaji yako sasa katika hilo kuna mambo kadhaa ya kuzungumzia na hatua ambazo tunazichukua.

Maelekezo

"Mtakumbuka Rais wetu alivyohutubia Bunge tarehe 22, Aprili 2021 mara tu baada ya kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi yetu alizungumzia kwamba serikali itapitia Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 na kupitia mitaala ili kuhakikisha kwamba tunaongeza ubora wa elimu na kuongeza ujuzi wa wale wanaosoma.

"Ili kuwaandaa vizuri ili waweze kuendesha maisha yao vizuri. Alisema angependa kuona elimu yetu inamwandaa mtu vizuri apate ujuzi akiingia kwenye mfumo wa uchumi anaweza akaendelea, Mheshimiwa Rais amerudia mambo hayo mara kadhaa.

"Na mimi alivyoniteua Wizara ya Elimu aliniambia alinipa maagizo hili niende nikalisimamie. Ningependa kuzungumzia mambo gani yanaendelea, huwa napenda kusema yajayo yanafurahisha. Kuna mambo saba ambayo ningependa kuyazungunzia na kuyafafanua.

Mambo muhimu

"La kwanza kabisa ni sera, tuna sera mbili ambazo tunazifanyia mapitio,kuna Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 na kuna Sera ya Sayansi na Teknolojia ya mwaka 1996 na hii ya Wizara ya Elimu Sayansi ya Teknolojia,pili ni Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 na hii sheria lazima iwe informed na sera kwa hiyo tukimaliza mapitio ya sera tunaona tutapitia na sheria ili sheria iwe nformed na sera na pia tuna sheria ya COSTEC ya mwaka 1984 ambayo tutaangalia namna ya kuibadilisha kwa sababu tunahitaji kuongeza tija kwenye masuala ya Sayansi na Teknolojia.

"Kuna masuala ya mitaala, sasa lazima mitaala iwe informed na sera, na sera ni kama farasi anavuta mkokoteni huwezi kutanguliza mkokoteni halafu uvute farasi, sera ndiyo inatoa direction yapo masuala mengine ya muhimu ambayo nitaendelea kuyasimamia moja kwa moja ikiwemo upatikanaji na kuwa na walimu, wakufunzi na wahadhiri wa kutosha kwa sababu unaweza kuwa na mitaala mizuri, kama hauna hao wasimamizi mambo yatakuwa bado.

"Pia tunahitaji hao walimu, wakufunzi na wahadhiri wawe na ubora stahiki na uwezo stahiki wa kwenda kufundisha. Sita tunahitaji miundombinu ya aina mbalimbali kwa ajili ya elimu na mwisho suala la.vitendea kazi,"anasisitiza Waziri Prof.Mkenda.

Utofauti sera

"Suala la Sera ya 2014 inaitwa Sera ya Elimu na Mafunzo ilifanyiwa kazi kwa muda mrefu sana, wataalam walisafiri walienda nchi mbalimbali Marekani, Ujerumani na Kenya kulikuwa na consultation (ushauri) kubwa sana kabla ya kupitisha hii sera 2014.

"Hii sera ikapitishwa bungeni ikashangiliwa kweli kweli katika mambo makubwa yaliyomo kwenye ile sera ni mfumo wa elimu ile sera inasema hivi Tanzania elimu ya lazima Compulsory Education itakuwa miaka 10 ambayo utagawanyika sehemu mbili miaka 6 ya basic education na miaka 4 ya secondary education.

"Lakini kila mtoto Mtanzania lazima asome hiyo miaka 10 kuanzia darasa la kwanza hadi la sita, halafu ataenda kidato cha kwanza, cha pili, cha tatu na cha nne hiyo ni sera ipo kwenye tovuti za Serikali kwa maana hiyo mfumo huu wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 unatambulika kama ni six, four, two three plus six basic education, four secondary education two high school three plus ukienda chuo kikuu ni miaka mitatu na kuendelea kutegemeana na unachosoma hiyo ndiyo sera ipo na haijawahi kufutwa.

"Kinachotekelezwa sasa hivi ni miaka saba ya Compulsory Education kwamba kila mtoto lazima asome miaka saba akishasoma miaka saba anaweza akaacha shule halazimishwi mzazi kwenda zaidi miaka saba.

"Mfumo unaotekelezwa sasa hivi ni seven, four, two na three plus kinachotokea sasa hivi ni tofauti na sera inachosema ndio maana Rais aliagiza fanyeni mapitio ya sera, kupitia sera ili sera yetu na tunachofanya kisitofautiane. Je? Tubadilishe tulichofanya kiendane na sera au sera ibadilike iendane na tunachofanya au tutafute kitu kingine."

"Hapo sasa kuna maswali ya kujiuliza, tunataka mtoto akimaliza shule aweze kujiajiri na aweze kuajirika na kelele kubwa katika elimu tunaona ni kwamba mtoto akimaliza shule hawezi kujiajiri, hawezi kujiariwa kwa mfumo wa seven, four, two na three plus mtoto aanze shule ana miaka 6 ukijumulisha 7 inakuwa 13 kwa hiyo watoto wetu wanatakiwa wamalize shule wakiwa na miaka 13 na hawalazimiki kuendelea, je? Mtoto wa miaka 13 anaajirika?." alihoji Prof. Mkenda.

Sheria

"Sheria za ILO ambazo sisi tumeziridhia zinasemaje kuhusu kuajirika ni umri gani mtu anaweza kuajiri. Ni muhimu sisi tuipitie sisi Tanzania tumetia saini katika makubaliano ya Dunia mkataba kutekeleza sustainable development goals walikuwa wakuu wa nchi na Tanzania sisi tulifanya hivyo goal namba 4 inasema ni kutoa free quality education up to secondary school, maana yake compulsory education inaendelea mpaka sekondari iwe free and quality education.

"Sasa tunapopitia sera lazima tujiulize tulichosaini kwa hiari yetu kinaendana na sera yetu? Lakini tunabadilisha kirahisi au lazima tutafakari vya kutosha.

"Nasema vitu ambavyo vinafanyiwa tafakuri, nilipoingia wizarani nilikuta kazi ya mitaala imeshaanza karibia mwaka mzima, na tulifanya mkutano Saint Gasper tukiita mashehe watu wenye shule binafsi chungu nzima walipopewa mhutasari wa yale yaliyomo kwenye mtaala takribani wote walisema Kamishna umetufilisi ndicho tulichokuwa tunataka zaidi ya maoni 100,000 yote yametoka kwenye mitaala sasa mitaala hii ilikuwa inafuata sera ipi.?

"Siyo Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ilikuwa inafuta kile kinachotekelezwa sasa hivi? Nikauliza kwa nini sera iko hivi na mitaala inakwenda hivi ilionekana ni gharama kutekelezwa hii sera ya 2014, gharama yake kiasi gani hilo halikufanyiwa.

Tume

"Tumeunda timu inayoongozwa na Prof. Joseph Sembojo mchuni na mle ndani kuna wachumi wawili wanaoweza kuchambua takwimu vizuri kazi yao kufanya mapitio ya sera hii na mle ndani tumemweka aliyekuwa Katibu wa Elimu wakati huo Prof. Mchome yeye anakumbukumbu watu walipoenda Ujerumani walijifunza nini, Marekani walijifunza nini.

"Ile timu inafanya kazi, inakusanya maoni sasa hivi ipo NACTE kupokea maoni wataenda Zanzibar na timu ina watu wa Zanzibar na huko itaenda nao kukusanya maoni katika yale ambayo tunataka wafanye moja ni watuandalie gharama hivi kama tukitekeleza sera ya 2014 maana yake nini kibajeti, na kama tukiamua kutekeleza itachukua muda gani kutekelezeka vizuri ili maamuzi itakapokuwa ikitekelezwa ifahamike tusije tukawa tunaogopa kutekeleza kumbe gharama sio kubwa au tukatekeleza kumbe gharama ni kubwa.

" Wenzetu Wakenya walikuwa kama sisi zamani walikuwa na seven, four, two, three plus mwaka 1980 wakabadilisha wakaenda eight, four, four plus wakati huo mtu wa Kenya akimaliza miaka 8 akaeda zake minne akija huku vyuo vikuu havimchukui kwa sababu Uganda na Tanzania wote tulikuwa na high school wakabadilisha Kenya wameenda six, three, three, na three plus.

"Nimeangalia Dunia nzima mwelekeo unakwenda siwezi kuzungumzia sasa hivi maamuzi...ukigoogle unaweza ukaangalia kila nchi compulsory education ni miaka mingapi, sasa hivi asilimia 73 wanaomaliza darasa la saba wanaendelea.

"Lakini la pili tunakwenda huko bila kushusha ubora wa elimu suala la kupanua ni moja, kwa sababu kila hatua tunapoenda ya kuongeza upatikanaji wa elimu ubora unashuka kidogo, UPE ulisaidia watu wengi, lakini ubora ukapungua kidogo shule za kata zimesaidia, lakini ubora umeshuka kidogo,"amesema Prof.Mkenda.

Ujuzi

"Ni nini kinahitajika ili tukienda huko tusishuke ubora, lakini kingine Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema elimu yetu iwe na sehemu kubwa ya kumuandaa mtu ujuzi, mfano uvuvi inakuandaa vipi kwenye uvuvi na pia hauwezi kuwa mvuvi tu inakuandaa vipi kwenye utandawazi, sababu tunajenga bomba la mafuta kutoka Uganda globalization (utandawazi) watu sasa hivi wanatafuta kazi na Congo DRC imeingia kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki, elimu hiyo inamwandaa vipi Mtanzania kuingia kwenye utandawazi na kukabiliana na changamoto za utandawazi.

"Mfano kuna dhana baada ya miaka sita basic education miaka minne inayofuata iwe na streams (mikondo) miwili siyo maamuzi, nasema tu mfano stream moja iwe ni ujuzi na nyingine academic...tunaweza kusema ujuzi uwe kwa kiwango kidogo na kikubwa academic haya siyo maamuzi, lazima tujiulize tunahitaji tuwekeze kiasi gani, tunahitaji kukusanya maoni tusifanye mambo kwa kukurupuka mpaka tukashusha ubora.

"Sasa tumalize kwanza sera, halafu tutakuja kwenye sheria kuna suala la tatu kwenye mitaala kama tukienda na sera ya 2014...vitu visijirudie rudie na haya ni maoni ya watu wengi sana mfano mwanafunzi anapofundishwa, mfano kimo cha mahindi au zao fulani asirudie tena tuondoe kujirudia rudia.

"Mtaala ni mkokoteni, utakuwa unavutwa na sera haiwezekani ukaanza na mtaala wakati sera hujaweka vizuri. Kazi ya mtaala inaenda mbali zaidi.Sasa hivi tumewaambia wajaribu kuangalia sera ya 2014 tuwe ready kama tutaendana na hiyo sera ama tutafanya modification (marekebisho) tuwe tayari kwenda vile, lakini kazi inakwenda vizuri sana.

Ufanisi

"Ukijaribu kuangalia shule ambazo zinafanya vizuri utakuta ina walimu wengi kuliko wanafunzi Arusha mfano...sisi tunasema walau mwalimu mmoja wanafunzi 45, Arusha wanafanya vizuri national avarege. Kuna sehemu mwalimu mmoja wanafunzi 104 Mkoa wa Kigoma baadhi ya Halmashauri Tabora Uyui mwalimu mmoja wanafunzi 74 unaweza ukaona performance ya wanafunzi ikoje, tunajaribu kuongea na wenzetu wa TAMISEMI mtu anaomba ajira anasema apelekwe kule akishapata tu anatafuta uhamisho apelekwe Dar es Salaam wakae kule kwa sababu kila mwanafunzi ana haki na anahitaji fursa ya kusoma.

"Na sasa hivi serikali imeanza kuajiri waalimu, jambo zuri sana tunaenda mbele, lakini vile vile tumepata fursa ya kuajiri wakufunzi na kadhalika na kutumia TEHAMA pengine tunaweza kufundisha sehemu nyingine mfano uchumi Masters ni somo hilo hilo kipindi cha COVID-19 lilifundishwa somo hilo hilo Tanzania, Ghana, Kenya kama una mwalimu wa Economy yuko Der es Salaam anaweza kufundisha UDOM.

Motisha kwa walimu

"Sababu kuwa na walimu ni jambo moja na kuwa na walimu bora ni jambo jingine, tunafufua zile zinazoitwa Teachers Resources Centre kuweza kuhakikisha wanabadilishana mawazo, wanapigana msasa tumeanza kufanya mafunzo rejea kwa walimu tulitumia shilingi bilioni 3 kufanya hivyo na mwaka huu tumeweka hela hizo hizo, unaweza ukachukua walimu wa hisabati wakaja wakabadilishana mawazo.

"Vile vile inawa-motivate, lakini kwenye vyuo vyetu vikuu vya Sayansi na Elimu tiba tumetenga shilingi bilioni moja mhadhiri yeyote ambaye atatoa chapisho lake, matokeo ya utafiti yakachapishwa kwenye majarida ya juu kabisa duniani mfano Nature anakitita chake cha milioni 50.

"Ataweza pengine kununua gari na kadhalika kuchapisha kule kuna maana unatoa mapendekezo ya kutatua changamoto. Wahadhiri wazuri ni wale wanaofanya utafiti ukimuacha anakuwa tu mwalimu wa high school kwa sababu University Job is to produce and to disciminate knowledge hii ni sehemu ya kuongeza ubora tunataka waende wafanye research.

"Tunatoa Scholarship sasa hivi kwa miradi kadhaa, kuna wakati watu walisema hatuwezi kupeleka watu nje ya nchi kusoma, tuna Vyuo vya Utalii nchini vingi vya binafsi na umma tunataka tuone ubora unasimamiwa TCU pia kwa vyuo vikuu lazima wasimamie ubora zile kanuni zipo anayesimamia anazijua na anayesimamiwa anazijua. Kama jambo ni baya aseme katika halmashauri tunaowadhibiti ubora wa elimu, kama kuna jambo waseme.

Miundombinu

"Kwenye miundombinu nako tunahitaji kuwekeza, lakini wakati wa Awamu ya Sita uwekezaji kwenye miundombinu ya elimu ni mkubwa sidhani kama tangu uhuru uwekezaji umekuwa mkubwa kiasi hiki, tumejenga zaidi ya madarasa 20,000.

"Unajua watu wengi wanataja madarasa yaliyojengwa na fedha za IMF ya UVIKO-19 madarasa 15,000 na shule shikizi 3,000 na ukiongea na wawakilishi wa wananchi (wabunge) kila mmoja atakwambia mimi kwangu kuna kitu kinaendelea.

Heshima kwa Rais

"Lazima tumpe credit, Mheshimiwa Rais Samia Hassan kwa sababu alipokwenda kuchukua fedha za UVIKO-19 alisema lazima ziache mark sio tunanunua barakoa au sanitazier...madarasa yameongezeka sana nchini na tuna-funds mbalimbali kwenye hii miaka mitano upo mradi wa CETIC trilioni 1.2 kati ya 2025 zaidi ya sekondari 1,000 kwa kipindi hicho ujenzi huu utakuwa na uhakika kuwabeba wanafunzi wote.

"Mradi wa BOOST una dola za Kimarekani milioni 200, huu utai-mprove quality education na vyuo vya serikali vitanufaika vipo vyuo pia cha Zanzibar (SUZA), sio hivyo tu tunapeleka kampasi kwa maelekezo ya Mheshimiwa Rais katika mikoa ambayo haina mfano Lindi, Kagera, Tabora, Mwanza Tanga, Ruvuma Mara Chuo cha Kilimo sha Mwalimu Nyerere tunatakiwa tukimalizie kimekaa muda mrefu sana.

"Pia VETA kila mkoa utakuwa na VETA tunajenga Njombe, Geita, Simiyu, Rukwa na Geita vinajengwa tunaelekea kujenga kila wilaya VETA shilingi bilioni 100 tumetengewa pia tunajenga Chuo cha TEHAMA tuna-location Dodoma.

"Pia tunajenga Chuo cha Ufundi Dodoma kitakachokuwa kama Dar es Salaam Institutes of Technology awamu ya kwanza kikikamilika mwezi wa 12 tunatarajia kitachukua wanafunzi 1,500 na awamu ya pili wanafunzi 3,000 wote wapate elimu kama inayotolewa na DIT na Arusha Tech.

Kompyuta kwa walimu

"Kwenye vitendea kazi tumeanza kampeni ya kugawa kompyuta na tukimaliza sensa vile vishikwambi tutavigawa vyote kwa walimu bora, kuanza kuona kwamba tutatumia TEHAMA ukiwa na tablet ile unaweza kusoma vitabu vyoote kwenye tablet moja na unaweza ukasoma ukafundisha suala la kuprint vitabu, gharama inaweza ikapungua hivyo itaanzia kwa walimu, lakini kwenye vyuo vya walimu kwa sasa nadhani tunaenda vizuri kila mwalimu anayesoma Chuo cha Ualimu Tanzania tutahakikisha anakuwa na kompyuta yake.

Vitabu

"Suala la vitabu bado ni pasua kichwa, vitabu vyetu bado vinachapishiwa nje ya nchi mfano Dubai, India...lakini kuna innovation moja lazima tujue ubora wa uandishi wa vitabu tumetenga fedha kwa ajili ya uandishi wa vitabu.

"Kwa mfano ukiandika riwaya ikiwa nzuri tunaongea na Pulisher tutainunua, hataogopa kupulish kwa sababu soko lipo tunapenda uwe uandishi wa kina wenye sanaa ndani yake na pia vinatunza utamaduni wetu na vinamleta mwanafunzi vizuri, hatusemi wasisome vitabu vya nje, bali kuchochea watu kuanza kuandika vitabu vizuri,"amefafanua kwa kina Prof.Mkenda ambaye ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news