NA MWANDISHI WETU
VIONGOZI wa wizara wametakiwa kufuatilia na kusimamia kwa karibu maafisa viungo ambao wanahusika kuweka taarifa kwenye mfumo ili viongozi wawe na umiliki (ownership) wa taarifa zilizo katika mfumo huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe.Geroge Simbachawene akizungumza katika kikao kazi cha Mawaziri kilichofanyika katika Ukumbi wa Kambarage Hazina jijini Dodoma.(Picha na OWM).
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene katika kikao kazi cha Mawaziri kilichofanyika katika Ukumbi wa Kambarage Hazina Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu akiwa katika Kikao kazi cha Mawaziri kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage hazina Jijini Dodoma.
“Kwa upande wa uwasilishaji wa
Taarifa ya Ilani ya Chama Tawala, uchambuzi umeonesha kuwa kwa kipindi
cha mwaka 2022 ni Wizara 14 zilizowasilisha Mpango Kazi wa Utekelezaji
wa Ilani kwa mwaka 2022 na Wizara 13 hazijawasilisha.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza jambo na Naibu Waziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete kabla ya kuanza kwa kikao kazi cha Mawaziri kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage jijini Dodoma.
"Kwa mwaka 2022 tumepokea maelekezo yako kuwa Taarifa ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhusu Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kuhusu Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 itawasilishwa mwezi Novemba, 2022.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bw. Kaspar Mmuya akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bw. Paul Sangawe katika kikao kazi cha Mawaziri kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage hazina Jijini Dodoma.
"Ili kuratibu taarifa hiyo vyema na kwa wakati, napenda Mawaziri kuratibu taarifa katika maeneo yanayowahusu na kuhakikisha zinawasilishwa kwa wakati kupitia mfumo huo,"alisema.