NA ABEL PAUL, Tanpol
JESHI la Polisi kupitia kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa mifugo nchini limesema linawashikilia watuhumiwa 15 waliohusika katika tukio la mauaji ya wafugaji katika Kijiji cha Mbatamila Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma.

Hayo yamesemwa Septemba 24, 2022 na Kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo na migogoro ya wakulima na wafugaji nchini, Kamishina Msaidizi wa Polisi, ACP SIMON PASUA alipofika Kijiji cha Mbatamila wilaya Tunduru Mkoa wa Ruvuma ambapo amebainisha kuwa jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa 15 kwa kosa la mauaji ya vijana wanne wa familia moja.
Ni katika Kijiji cha Mbatamila na kusema kuwa wale wote waliofanya mauaji hayo hawako salama na kuwataka wajisalimishe Jeshi la Polisi.
.jpeg)
Sambamba na hilo amewapa pole wananchi waliopoteza ndugu zao ambapo Kamanda Pasua amesema, jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wote walio baki ili wafikiahwe katika vyombo sheria kujibu tuhuma zinazowakabili.
MIFUGO 159

Pia Kamanda Pasua amesema kuwa, jeshi hilo limefanikiwa kukamata mifugo 159 iliyokuwa imeibiwa katika Kijiji cha Mbatamila Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wafugaji Nchini, Bi. Prisca Kaponda amesema, wao kama chama cha wafugaji kitaendelea kutoa elimu kwa wafugaji juu ya matumizi bora ya ardhi ili kumaliza migogoro ya wakuliama nawafugaji hapa nchini.
.jpeg)