NA DIRAMAKINI
WATU watano wamefariki huku 54 wakijeruhiwa katika ajali ya basi la abiria kugongana na Fuso uso kwa uso eneo la Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
WATU watano wamefariki huku 54 wakijeruhiwa katika ajali ya basi la abiria kugongana na Fuso uso kwa uso eneo la Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Manusura wa ajali hiyo Fred Mahina, amesema dereva wa basi hilo alikuwa akiendesha mwendokasi na walipokuwa wakimzuia aliwajibu wangetaka usafiri wa raha wangepanda ndege, huku akiwaambia wasali sana ili wafike salama.
"Tulipofika Morogoro dereva akiwa mwendokasi alikwaruza Roli tukapona kuanguka, lakini akazidi kuendesha mwendokasi abiria tulipokuwa tukipiga kelele apunguze mwendo, aligoma na kutuambia tusali ,ndipo tulipofika hapa Shinyanga na kupata ajali," anasema Mahina.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Leonard Nyandahu ambaye alikuwa eneo la ajali hiyo, amesema chanzo ni uzembe wa dereva wa basi kwa kutozingatia vibao vya usalama barabarani na kuendesha mwendokasi.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga, Dkt. Luzila John amethibitisha kupokea vifo vya watu watano pamoja na majeruhi 54 ambao wanaendelea na matibabu.