Al-Mustafa International University waonesha utayari kuwekeza Zanzibar

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Septemba 10,2022 amekuwa na mazungumzo na ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha Al-Mustafa (Al-Mustafa International University) kutoka nchini Iran.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungunza na Ujumbe wa Uongozi wa Chuo Kikuu cha Al-Mustafa kutoka nchini Iran ukiongozwa na Rais wa chuo hicho, Dkt.Ali Abbasi,mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo.

Ujumbe huo ulioongozwa na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran nchini Tanzania, Hossein Alvandi Bahiney ulikutana na Rais Dkt.Mwinyi, Ikulu jijini Zanzibar ikiwa ni mwendelezo wa mazungumzo kati ya Rais na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir Abdollahian yaliofanyika Ikulu Zanzibar, Agosti 26 mwaka huu.

Mazungumzo yakiwa na lengo la kukuza ushirikiano kati ya nchi mbili hizo kupitia sekta za Elimu, Afya, Sayansi na Teknolojia, Viwanda pamoja na Uchumi wa Buluu.

Katika mazungumzo hayo Rais wa Chuo Kikuu cha Almustafa, Dkt.Ali Abass alibainisha azma ya Uongozi wa Chuo hicho kushirikiana na Serikali ya Zanzibar kuanzisha tawi la chuo hicho hapa nchini.

Akizungumzia suala hilo, Rais Dkt.Mwinyi aliishukuru Serikali ya Iran kwa hatua hiyo inayolenga kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya nchi mbili hizo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi mgeni wake, Rais wa Chuo Kikuu cha Al-Mustafa cha nchini Iran, Dkt. Ali Abbasi baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyoyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo na kulia kwake ni Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mhe.Hossein Alvandi Bahineh.(Picha na Ikulu).

Alitumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa chuo hicho kwa uharaka wake katika kuendeleza mazungumzo yalioasisiwa na Waziri Amir, wiki mbili zilizopita wakati viongozi hao walipokutana.

Aidha, Dkt.Mwinyi alibainisha utayari wa Serikali katika kushirikiana na uongozi huo kuendeleza sekta ya elimu nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news