CCM, CUF wapeleka wabunge tisa EALA

NA DIRAMAKINI

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limewachagua wawakilishi tisa kwenye Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwezi Desemba, mwaka huu.

Akitangaza majina ya washindi wa uchaguzi wa wawakilishi hao Septemba 22, 2022 bungeni jijini Dodoma, Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson amewataja kuwa ni pamoja na Angela Kizigha ambaye ameshinda kwa kipindi cha pili, Nadra Juma Mohamed na Dkt.Shogo Mulozi.

Wengine waliochaguliwa ni Abdulla Hasnuu Makame ambaye amechaguliwa kwa kipindi cha pili, Machano Ally Machano na Aswar Kachwamba.

Wawakilishi wengine ni aliyewahi kuwa Mbunge wa Simanjiro James Ole Millya, Dkt.Ng’waru Maghembe huku nafasi ya uwakilishi kwa walio wachache ikichukuliwa na mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Mashaka Khalfan Ngole.

Miongoni mwa wagombea walioangukia pua kwenye kinyang’anyiro hicho ni Ado Shaibu ambaye ni Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo akizidiwa kura na Mashaka wote kutoka vyama vichache vyenye uwakilishi bungeni.

Wakati huo huo, Spika Dkt.Tulia amewataka wawakilishi hao kuhakikisha wanatanguliza maslahi ya Taifa mbele na wasiende na mawazo yao binafsi.

Mheshimiwa Spika Dkt.Tulia amesema kuwa, uwepo wa wabunge hao katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ni uwakilishi wa Watanzania, hivyo wanapaswa kuongozwa na falsafa za Watanzania kwa matokeo chanya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news