Dkt.Ndonde atoa wito kwa wasindikaji wa chakula nchini

NA IMMA MSUMBA

WASINDIKAJI wa vyakula pamoja na wafanyabiashara wametakiwa kuwa na utaratibu unaoonesha mchanganyiko unaotumika katika bidhaa zao ili kumruhusu mlaji kufanya maamuzi kabla ya kufanya manunuzi na kujiepusha na magonjwa yasiyoambukiza yanayotokana na baadhi ya vyakula.
Mtaalamu wa Afya na Mazoezi kutoka Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukiza, Dkt. Waziri Ndonde akizungumza jijiji Arusha wakati wa majadiliano ya kufikisha elimu kwa jamii namna ya kujiepusha na tabia bwete na ulaji wa vyakula usiozingatia viwango amesema, watu wengi ununua vyakula bila kuzingatia mchanganyiko uliopo na kupata athari.
Dkt. Ndonde amesema kuwa, kwa sasa wanafanya tafiti zitakazosaidia kuondokana na kasi ya kuenea kwa magonjwa yasiyoambuliza yanayosababishwa na matumizi ya vyakula visivyofaa.

Pia Dkt.Ndonde ameongeza kuwa, namna pekee itakayosaidia kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari pamoja na magonjwa ya moyo ni pamoja na kuacha tabia bwete na kuanza kufanya mazoezi ikiwa ni njia pekee ya kupunguza athari zitokanazo na matumizi ya vyakula.
Hata hivyo, Dkt.Ndonde amesema ipo haja ya mamlaka zinazosimamia chakula na dawa kutunga sheria madhubiti pamoja na kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya vyakula na dawa ikiwa ni mpango wa kusaidia afya ya jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news