NA DIRAMAKINI
MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini kuwa kumekuwa na ukosefu wa maji kutokana na changamoto ya umeme iliyojitokeza kuanzia asubuhi ya tarehe 27.09.2022.
Hitilafu hiyo imesababisha mtambo kutoweza kufanya kazi hivyo kupelekea upungufu wa huduma ya maji katika mji wa Bagamoyo na sehemu kubwa ya mkoa wa Dar es salaam.
Maeneo yanayoathirika ni pamoja na; Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Mbweni, Boko, Salasala, Kunduchi, Mbezi Beach, Goba, Mivumoni, Madale, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo Kikuu, Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala na Katikati ya mji.
Mafundi wa TANESCO wanaendelea na jitihada kuhakikisha huduma ya umeme inarejea.
Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au
0735 202-121(WhatsApp tu)
Tovuti: www.dawasa.go.tz
Mitandao ya kijamii.
Facebook: https://www.facebook.com/pg/Dawasaofficial/posts/
Instagram: https://instagram.com/dawasatz?utm_medium=copy_link
Twitter: https://twitter.com/dawasatz?s=08
YouTube: https://youtube.com/channel/UCCVyHKIvUwDFG1tUyWhd7fQ
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano na Jamii