NA TITO MSELLEM-WM
JUKUMU la Wizara ya Madini ni kuunda Sera na kusimamia Sheria ya Sekta ya Madini sambamba na utoaji wa mafunzo ya kitaalamu ya uendeshaji wa shughuli za madini ikiwa ni pamoja na kusimamia taasisi zilizo chini ya wizara.

Mbibo amesema lengo la semina hiyo ni kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata elimu na ujuzi wa namna bora ya utafiti, uchukuaji wa sampuli, uchimbaji na uchenjuaji wa madini.

"Ili Sekta ya Madini iweze kutunufaisha ipasavyo, lazima tuyafanye kwa uzuri na kwa utaratibu ikiwemo kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu," amesema Mbibo.

Pia, Mbibo ameiagiza Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuendelea kutoa elimu ya namna ya kufanya tafiti na uchukuaji wa sampuli.
Sambamba na hayo , Mbibo ameupongeza mkoa na wilaya ya Geita kwa kuendesha zoezi la uandaaji wa Maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini 2022.
Katika hatua nyingine, Mbibo ametembelea maandalizi ya Maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini katika mabanda yote yanayoendelea mkoani Geita.