
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusiana na masuala ya serikali Mtandao, mara baada ya eGA kutoa mafunzo ya usalama wa serikali mtandao kwa wajumbe wa kamati hiyo.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Kusini Unguja (CCM) Mhe. Mwantumu Dau Haji akichangia hoja kuhusu serikali mtandao, mara baada ya kupatiwa mafunzo ya usalama wa serikali mtandao yaliyotolewa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).
