NA SOPHIA FUNDI
WENYEVITI wa mamlaka ya Mji mdogo Halmashauri ya Wilaya ya Karatu mkoani Arusha wametakiwa kusimamia fedha za Serikali zilizoelekezwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika maeneo yao.
Akizungumza na wenyeviti hao katika kikao cha Baraza la Mamlaka ya Mji mdogo wa Karatu, Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Dadi Kolimba alisema kuwa, Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo, hivyo ni jukumu la wenyeviti kusimamia fedha hizo zitumike kama zilivyoelekezwa.
Alisema kuwa ,ni Jambo la kuishukuru Serikali kwa kutoa fedha za ruzuku kiasi sha shilingi bilioni 1.7 mapema kwani fedha hizo zitatumika kukamilika miradi mbalimbali na zilikuwa hitaji la Wanakaratu.
Kwa upande wake mwenyeiti wa mamlaka ya Mji mdogo Karatu, Yuda Morata akizungumza katika kikao hicho alisema wao kama wenyeviti wamepokea maelekezo ya serikali na watahakikisha fedha hizo wanazisimamia na kutumia kwa malengo husika.
Kwa niaba ya wenyeviti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu ameshukuru serikali kutoa fedha hizo za ruzuku kwani itasaidia wananchi wao kuwapunguzia michango mbalimbali kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Aliwaomba wenyeviti kuhakikisha wanajua miradi ambayo iko kwenye maeneo yao na kusimamia fedha zilizotolewa na serikali.