Makamu wa Rais Dkt.Mpango asisitiza maadili mema kwa vijana

NA MUNIR SHEMWETA-WANMM

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Phillip Mpango amewataka viongozi wa dini nchini kuwafundisha na kulea vijana katika maadili mema pamoja na kuthamini kufanya kazi kihalali.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula akimsalimia Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus Ruwa’ichi wakati wa Jubilee ya miaka 25 ya Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Kibiti na sherehe za kutabaruku kanisa na Altare iliyofanyika Kibiti mkoani Pwani ambapo alimwakilisha Makamu wa Rais, Dkt.Phillip Mpango tarehe 25 Septemba 2022.

Dkt.Mpango amesema hayo leo Septemba 25, 2022 katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula katika Jubilee ya miaka 25 ya Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Kibiti na sherehe za kutaburuku kanisa na Altare iliyofanyika Kibiti mkoani Pwani.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Dkt.Angeline Mabula akizungumza katika Jubilee ya miaka 25 ya Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Kibiti na sherehe za kutabaruku kanisa na Altare iliyofanyika Kibiti mkoani Pwani ambapo alimwakilisha Makamu wa Rais, Dkt.Phillip Mpango leo Septemba 25,2022.

Amesema, katika nyakati hizi ni ukweli ulio wazi kuwa kuna mmomonyoko wa maadili katoka jamii, vitendo viovu na mambo yasiyompendeza Mungu kuzidi kuongezeka mambo aliyoyaeleza kuwa siku za nyuma yalikuwa nadra sana kutokea au kusikika na hivi sasa yanakuwa habari za kila siku na wakati mwingine huonekani ni kawaida.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akivishwa Skafu na Skauti wakati wa Jubilee ya miaka 25 ya Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Kibiti na sherehe za kutaburuku kanisa na Altare iliyofanyika Kibiti mkoani Pwani ambapo alimwakilisha Makamu wa Rais, Dkt.Phillip Mpango leo Septemba 25,2022.

Kwa mujibu wa Dkt.Mpango, kushuka kwa maadili ni jambo lenye athari mbaya kwa jamii na taifa kwa ujumla hivyo kunachangia kurudisha nyuma juhudi za kujiletea maendeleo nchini na kufanya kazi ya kuondoa umasikini kuwa ngumu.

Kupitia hotuba ya Makamu wa Rais, Dkt.Mabula amesema, anaamini watu pamoja na viongozi wa serikali na wa vyama vya siasa wakishika mafundisho ya dini pamoja na kuwa na hofu ya mungu maovu mengi yatapungua na nchi kuongozwa vizuri.

Kufuatia hali hiyo, ameomba kwa niaba ya serikali viongozi wa dini wasaidie kulea taifa kimaadili na kuweka mkazo zaidi kwa vijana kwa kuwa wao ni wahanga wakuu wa maovu yanayotendeka na pia ni viongozi wa kesho.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akimkabidhi Risiti ya Benki ikiwa ni Mchango wa Makamu wa Rais Dkt.Phillip Mpango alioutoa kwa ajili ya maendeleo ya ujenzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Kibiti kwa Pande Christian Lupindu leo Septemba 25, 2022.

"Tukiwaandaa vyema vijana wetu mustakabali wa taifa letu na watu wake utakuwa kwenye mikono salama na tukishindwa leo tutalia na kusaga meno kesho, uhai wa taifa letu utakuwa mashakani,"amesema Dkt.Mpango.

Kupitia hotuba hiyo Dkt.Mpango pia alisisitiza suala la usafi na utunzaji mazingira ambapo aliwaomba viongozi wa kanisa katoliki na madhehebu mengine ya dini kupaza sauti kuhamasisha , ulinzi na uhifadhi wa mazingira katika nchi.

"Katika dini zetu Mwenyezi Mungu alitupatia dunia nzuri na akatuamuru tuitunze, niwaombe ninyi mlio mawakala wa mwenyezi mungu hapa duniani muwaongoze waumini na kuwahimiza kuitunza ekolojia ya nchi yetu nzuri kwa kutunza misitu na vyanzo vya maji , kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira wakati wote,"amesema Dkt.Mpamgo.
Sehemu ya washiriki katika Jubilee ya miaka 25 ya Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Kibiti na sherehe za kutaburuku kanisa na Altare iliyofanyika Kibiti mkoani Pwani leo Septemba 25,2022.

Kuhusu mimba na ndoa za utotoni, Dkt.Mpango aliwaomba viongozi wa dini kukemea mimba na ndoa za utotoni kwa kuwa ni kinyume cha sheria na maadili ambapo alieleza kuwa suala hilo linawanyima fursa watoto wa kike kusoma na kufikia malengo sambamba na kusababisha matatizo ya fistula kwa watoto wa kike na kusisitiza watoto wa kike waachwe wasome ili waweze kufikisha malengo yao.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus Ruwa’ichi aliwapongeza wana Kibiti kwa kuwa na kanisa lililokamilika na kuwashukuru wote walioshirikiana katika ujenzi wa kanisa hilo.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Jude Thaddaeus Ruwa’ichi katika ibada ya kutabaruku Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Kibiti iliyofanyika Kibiti mkoani Pwani leo Septemba 25, 2022. Kulia ni Padre wa Kanisa hilo, Christian Goya Lupindu.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).

Amesema, ujenzi wa kanisa hilo umechukua muda wa miaka 11 na kueleza kuwa, muda huo umekuwa muda wa kukomaa na kuwataka wana kibiti kuonesha ukamavu na kumpongeza Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Kibiti Christian Goya Lupindu kwa kujituma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news