NA DIRAMAKINI
JAMHURI ya Muungano wa Tanzania na China zimeadhimisha urafiki wa miaka zaidi ya 50 ambao umeleta mafanikio katika sekta mbalimbali ikiwemo Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Amesema, mchezo wa mpira wa meza ni miongoni mwa michezo inayokua hapa nchini, na Serikali inaendelea kuwekeza katika mchezo huo ambao unakuza vipaji na kutengeneza ajira kwa vijana.
“Mpira wa Meza unachezwa sana na wanafunzi katika shule za Msingi na Sekondari, na katika Mashindano ya Michezo kwa shule hizo pamoja na Vyuo vya Ualimu na Taasisi za Umma pia unachezwa na unaleta ushindani Mkubwa, hivyo ni miongoni mwa michezo inayotangaza nchi vyema” alisema Ndugu Saidi Yakubu.
Ametumia nafasi hiyo kuliagiza Baraza la Michezo nchini, kukaa na Ubalozi wa China kushirikiana na kuratibu kwa karibu zaidi matukio yote ya michezo yanayoshirikisha nchi hizo, ili kuweza kupata wachezaji wengi zaidi watakaoshindana.

Mhe.Chen Ming Jian amesema China imedhamiria kujenga kiwanda Cha kuzalisha filamu, kubadilishana wataalamu katika sekta ya Michezo na Utamaduni na imeahidi kushiriki katika Tamasha la 41 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo.
Mashindano hayo yameandaliwa kwa ushirikiano kati ya Umoja wa wacheza mpira wa Meza Tanzania na China pamoja na kituo cha Utamaduni cha China.