NA DIRAMAKINI
SERIKALI imesema haina mpango wa kubadili utaratibu uliowekwa kwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa kukaa miaka sita bila kuoa ama kuolewa mara baada ya kujiunga na jeshi hilo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dkt.Stregomena Tax wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Bunda, Boniface Getere aliyetaka kufahamu Serikali ina mpango gani wa kupunguzwa kwa miaka sita iliyopo kwa sasa kwa askari wapya wa jeshi kuoa ama kuolewa na kuwa mwaka mmoja ama miaka miwili.
Dkt.Tax amesema kuwa, kwa sasa utaratibu huo utabakia kama ulivyo kutokana na misingi iliyowekwa kwa ajili ya kuwaandaa askari hao kulinda nchi.
Amesema, askari wapya wanaojiunga na jeshi wanahesabiwa kama wapiganaji ambao wanapaswa kupewa ujuzi zaidi na kutumika kwenye vita, hivyo miaka sita iliyowekwa ya kutokuoa ama kuolewa inatoa nafasi kwa askari hao kutumika katika shughuli za medani.