NA MWANDISHI WETU
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bahati Geuzye amesisitiza umuhimu wa watendaji wa halmashauri nchini kushirikiana na TEA katika usimamizi wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu inayofadhiliwa na Mfuko wa Elimu wa Taifa unaoratibiwa na TEA katika maeneo yao ili itekelezwe kwa ufanisi
Mkurugenzi Mkuu wa TEA alikuwa akitoa wasilisho katika Mkutano Mkuu wa 36 wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT) unaofanyika jijini Mbeya.
Amesema, katika mwaka wa fedha 2022/2023 kiasi cha Sh.bilioni 8.9 zimetengwa kwa ajili ya kufadhili miradi ya ujenzi wa miundombinu katika sehemu mbali mbali nchini
Miradi hiyo itahusisha ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo, nyumba za walimu na miudombinu ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.