'MRADI WA MAJI BUTIMBA NI CHACHU KATIKA KUENDELEZA UHIFADHI'

NA HAPPINESS SHAYO-WMU

CHANZO cha Maji na Kituo cha Tiba ya Maji cha Butimba chenye thamani ya shilingi bilioni 69.3 ni chachu ya kuendeleza shughuli za uhifadhi zitakazosaidia kuongeza idadi ya watalii nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi wa kituo hicho katika Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza.

“Mradi huu unaenda kuimarisha uhifadhi katika Sekta yetu ya Maliasili kwa kuwa tunapotunza na kuhifadhi vizuri vyanzo vya maji utalii nao utaenda vizuri kwa sababu tutakuwa na mazingira yanayovutia,”Mhe. Masanja amesisitiza.

Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya mradi huo unaoenda kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wanawake wa hususan mkoa wa Mwanza.

“Mradi huu unaenda kupunguza muda mwingi uliokuwa ukitumiwa na wanawake kutafuta ili kuhudumia familia zao” Mhe. Masanja amefafanua.

Mradi wa Maji wa Butimba umewekewa jiwe la Msingi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango Septemba 14,2022 .

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news