MWENYEKITI GEREMA NYANG'HWALE ATAKA WAFANYAKAZI OFISI ZA MADINI KUONGEZWA

NA DIRAMAKINI

MWENYEKITI wa Chama cha Wachimbaji Wadogo (GEREMA) Wilaya ya Nyang'hwale Misala Jeremiah amesema kuwa changamoto kubwa inayowakumba wachimbaji wadogo ni upungufu wa watumishi katika Ofisi za madini na kusababisha baadhi ya huduma kutopatikana kwa wakati.
Misala Jeremiah,Mwenyekiti wa Gerema Wilaya ya Nyang'hwale

Jeremiah amesema hayo Septemba 28,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Maonyesho ya teknolojia ya madini yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili mjini Geita katika eneo Maalum la uwekezaji (EPZ).

Amesema kuwa, pamoja na upungufu wa watumishi, pia waliopo wanakabiliwa na upungufu wa vyombo vya usafiri hivyo kuwa changamoto ya kufika katika maeneo ya wachimbaji kutoa huduma.
Mhandisi John Kalimenze, Mkuu wa GST Mkoa wa Geita.

Ameiomba serikali kuongeza wafanyakazi wa Ofisi za madini pamoja na kuongeza vyombo vya usafiri ili wachimabaji wadogo waweze kuhudumiwa kikamilifu na Kwa wakati.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Geita Wilson Shimo alimuomba Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo kushughulikia upungufu wa watumishi.

Naibu katibu mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo akizungumza katika Maonyesho hayo amesema wizara hiyo imejipanga kushughulikia changamoto zote zinazo wakabili wachimbaji wadogo nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news