NBC yazindua msimu wa pili kampeni kwa wakulima wa korosho

NA DIRAMAKINI

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua msimu wa pili wa kampeni yake maalum kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi inayofahamika kama 'Vuna zaidi na NBC Shambani' ikilenga kuunga mkono na kufanikisha adhma ya serikali ya kuzalisha tani 700,000 za zao hilo kwa mwaka ifikapo mwaka 2025.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya (wanne kushoto) akioneshwa moja ya simu janja (smart phone) na Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo wa benki ya NBC Bw Elibariki Masuke (wa tatu kulia) ikiwa ni sehemu ya zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwa washindi wa msimu wa pili wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Mtwara leo. Wanaoshuhudia ni pamoja na viongozi waandamizi wa benki ya NBC pamoja na wadau wengine wa zao korosho mkoani Mtwara.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya ameongoza hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika mkoani humo Septemba 29, 2022 na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa zao hilo wakiwemo viongozi wa kiserikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS) na vyama vikuu vya ushirika maofisa wa benki wa Benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo wa NBC Bw Elibariki Masuke.
Wadau mbalimbali wa zao la korosho mkoani Mtwara wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika mkoani humo wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.

Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Bw Kyobya alisema imekuja wakati muafaka kwa kuwa inakwenda sambamba na mpango wa serikali wa kuhakikisha sekta ya kilimo inachangia pato la taifa kwa asilimio 10 ifikapo mwaka 2030.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya (katikati) akijaribu ubora wa moja ya matrekta ambayo ni miongoni mwa zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa msimu wa pili wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Mtwara leo. Wanaoshuhudia ni pamoja na viongozi waandamizi wa benki ya NBC akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke (wa tatu kulia) pamoja na wadau wengine wa zao korosho mkoani Mtwara.

“Na ndio sababu nawapongeza sana Benki ya NBC kwa mkakati huu ambao hapo tu kimasoko bali pia unaunga mkono jitihada za serikali kukuza sekta hii muhimu na pia inalenga kumkomboa mkulima. Wito wangu kwa wakulima wa korosho mkoa wa Mtwara na Lindi naomba sana tuwaunge mkono NBC kwenye hili,’’ alisisitiza.

Akizungumzia zawadi mbalimbali zinazotolewa kupitia kampeni hiyo ikiwemo trekta, maguta (Toyo), baiskeli, pikipiki, pampu za kupulizia dawa simu janja, kanga, mabegi na madaftari, Bw Kyobya alisema zinalenga kuunga mkono jitihada za mkulima katika kuboresha kilimo na uzalishaji hatua ambayo ina tija zaidi kiuchumi katika mkoa huo.
Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo wa benki ya NBC,Bw Elibariki Masuke akizungumza na wadau mbalimbali wa zao la korosho mkoani Mtwara wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika mkoani humo wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Mtwara.

“Msisitizo wangu tu kwa wakulima ni suala zima la nidhamu ya fedha na kutumia vema mafunzo yanayotolewa na benki ya NBC kuhusu umuhimu wa kujiwekea akiba, matumizi ya bima mbalimbali ikiwemo bima ya afya pamoja na kuwekeza kwenye zana za kisasa za kilimo,"alisema.

Kwa upande wake Bw Masuke alisema msimu wa pili wa kampeni hiyo ya miezi mitatu ni muendelezo wa mkakati wa benki hiyo wa kujidhatiti kwenye kuinua kilimo cha mazao ya kimkakati ikiwemo zao la Korosho kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara.
Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa akizungumza na wadau mbalimbali wa zao la korosho mkoani Mtwara wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika mkoani humo wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Mtwara.

“Tunashukuru kuona kwamba kampeni yetu ya mwaka jana ilipokewa vizuri sana na wakulima wa korosho katika mikoa hii ya Lindi na Mtwara na zaidi tunajivunia kuona kwamba kampeni ile ilimalizika kwa mafanikio kwa wakulima ambapo tuliweza kukabidhi kwa wakulima zaidi ya 150 ambapo tulikabidhi jumla ya pikipki 25, pampu za umwagiliaji zaidi ya 60, baiskeli 70, na trekta 1. Ni matumaini yetu mwaka huu mambo yatakuwa mazuri zaidi’’ alitaja.

Alisema katika kampeni ya mwaka huu wakulima hao pia watakuwa kwenye nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo baiskeli, pikipiki, pampu za kupulizia dawa na zawadi za kifamilia ikiwemo simu janja, kanga, mabegi na madaftari .’’
Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Kusini Bi Zubeider Haroun akizungumza na wadau mbalimbali wa zao la korosho mkoani Mtwara wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika mkoani humo wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Mtwara.

“Kwa upande wa wa vyama vya msingi (AMCOS) vinaweza kujishindia zawadi kubwa zaidi ikiwemo maguta (Toyo) pamoja na matrekta,ili walengwa hawa wote waweze kujishindia zawadi hizi wanatakiwa wafungue akaunti benki ya NBC na wapitishe fedha za malipo yao kwenye akaunti hizo na moja kwa moja watakuwa wameingia kwenye droo ya kujishindia zawadi hizi,’’alifafanua.

Wakizungumzia kampeni hiyo pamoja na mpango wa NBC Shambani kwa ujumla, viongozi wa AMCOS katika mkoa huo walisema umekuwa na tija kubwa kwa wakulima huku wakionesha kuvutiwa zaidi na suala la kutokuwepo kwa makato ya fedha zao pindi wanapopitisha fedha hizo kupitia akaunti zao za NBC Shambani.
Meneja wa benki ya NBC Tawi la Mtwara Bi Editha Mwakatobe akizungumza na wadau mbalimbali wa zao la korosho mkoani Mtwara wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika mkoani humo wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Mtwara.

“Pamoja na uwepo wa zawadi mbalimbali kwenye kampeni hii ambazo kimsingi zitavutia wakulima wengi zaidi kujiunga na benki ya NBC zaidi tunavutiwa na kutokuwepo kwa makato ambayo yamekuwa yakituumiza sana hasa sisi viongozi wa AMCOS pindi tunapopitisha fedha za wanachama wetu kupitia akaunti zetu…kupitia akaunti za NBC Shambani tunashukuru kuona kwamba changamoto hii imekwisha kabisa,’’ alisema Bw Juma Hamadi Saidi ambaye ni Katibu wa AMCOS ya Tandahimba.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya (Katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa zao la korosho mkoani Mtwara wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa Benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke (wa tatu kushoto walioketi), viongozi vyama vya msingi (AMCOS), vyama vikuu vya ushirika mkoani humo wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika mkoani Mtwara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news