NA LWAGA MWAMBANDE
LIGI Kuu ya Soka ya NBC Tanzania Bara ambayo ina udhamini mnono kutoka Benki ya NBC na wadau wengine nchini, imeendelea kuwa na mvuto na ushindani wa kipekee.
Kila klabu au timu ambayo imefanikiwa kuingia katika ligi hiyo, inapambana kufa na kupona bila kujali ukubwa au udogo wa wapinzani wao, dhamira ikiwa ni kupata matokeo ambayo yatawawezesha kusonga mbele ili mwisho wa siku waweze kuingia katika hatua nzuri kama si kutwaa taji.
Mshairi wa kisasa, Bw.Lwaga Mambande anasema kuwa,katika ligi hii haupaswi kujivunia ukubwa au umaarufu wako, kwani lolote linaweza kutokea na mwishowe, ukaambulia aibu huku yule ambaye ulimuona ni mdogo au mchanga akasonga mbele, jifunze jambo kupitia hapa chini;
Ligi yetu kuongoza, bila kufanya makossa,
Walikuwa ni wa kwanza, wakubwa walinyanyasa,
Ndani ya kokwa la embe, dudu laweza ingia.
2.Kuja Tukuyu Stars, nchi waliitikisa,
Mpira ni kama kazi, ubingwa wakaunasa,
Kweli walifanya kazi, bila kufanya makossa,
Ndani ya kokwa la embe, dudu laweza ingia.
3.Chini ya mlezi Kaka, mpira ligusagusa,
Walicheza bila shaka, timu zingine kutesa,
Mwaka mosi kaibuka, vigogo wakatikisa,
Ndani ya kokwa la embe, dudu laweza ingia.
4.Huko Aston Pardon, kiungo alinyanyasa,
Godwin Aswile ndani, beki hatari kitasa,
Ugali si bilingani, ule walikula hasa,
Ndani ya kokwa la embe, dudu laweza ingia.
5.Miaka kadha kupita, Pamba nayo linyanyasa,
TP Lindanda ukuta, ni zaidi ya Pawasa,
Magwiji wengi lipita, hawakufanya makossa,
Ndani ya kokwa la embe, dudu laweza ingia.
6.Wagosi wa Kaya pia, kuna mwaka walitesa,
Bingwa si kushikilia, ingawa walitikisa,
Fainali liingia, Frika Mashariki hasa,
Ndani ya kokwa la embe, dudu laweza ingia.
7.Mtibwa ninawataja, hawa wananesanesa,
Ubingwa waliuonja, kuupata na kuukosa,
Walivyotembeza kwanja, Manungu siyo Kilosa,
Ndani ya kokwa la embe, dudu laweza ingia.
8.Ni wengi wa kukumbuka, Simba Yanga liwatosa,
Ubingwa wakaushika, na kwa makwapa fursa,
Cosmopolitan daka, Na timu ya Pan hasa,
Ndani ya kokwa la embe, dudu laweza ingia.
9.Hivi karibuni ona, Azam litesatesa,
Wakazama tunaona, sera zao liwatosa,
Lakini sasa twaona, wameshapania hasa,
Ndani ya kokwa la embe, dudu laweza ingia.
Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602
ITAENDELEA...