NA GODFREY NNKO
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limesema hivi karibuni linatarajia kuanza ujenzi wa nyumba za bei nafuu katika eneo la Kawe Tanganyika Packers lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kawe Tanganyika Packers ni miongoni mwa maeneo yenye historia ndefu nchini ambapo licha ya historia hiyo pia limekuwa maarufu zaidi kutokana na huduma za neno la Mungu ambalo huwa linatolewa hapo na watumishi mbalimbali akiwemo Mtume na Nabii, Boniface Mwamposa wa Arise And Shine Ministries.
Hayo yamesemwa Septemba 2, 2022 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu wakati akiwasilisha mipango waliyonayo kwa wadau wa Sekta ya Milki nchini.
Ni kupitia mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambao ulianza Septemba Mosi hadi 2 na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta hiyo nchini.
Bw.Mchechu amesema, wanafanya jitihada hizo kwa kuzingatia kwamba, Tanzania inakadiriwa hadi kufikia 2100 huenda ikawa kati ya mataifa 10 yenye watu wengi duniani, hivyo suala la makazi bora na nafuu halikwepeki.
"Tutakuwa na idadi kubwa ya watu,hivyo tunapozungumza namba hii tunazungunza vitu viwili kitu cha kwanza tuna wajibu wa kuwa na mipango thabiti ambayo itaweza kusaidia Taifa hili kumudu hiyo idadi kubwa ya watu.
Wadau mfahamu
"Pili kwa wadau wa sekta hii ambayo tumekutana (wadau wa Sekta ya Milki Tanzania) tunapaswa kufahamu kuwa, katika soko letu kuu sekta hii itaendelea kukua na tuna soko kubwa, kwa hiyo tujipange namna ya kulichangamkia hili soko kubwa na kuwaza kulitumia kwa sababu hawa watoto wanaozaliwa na wanaoongezeka watahitaji makazi.
"Na sisi ndio wazalishaji wa makazi. Juu ya suala la wakazi wa mijini ukiangalia mwaka 2000 Afrika ilikuwa ndio bara la pili kutoka mwisho kwa kuwa na watu wengi wanaoishi mjini.
"Kwa mwaka 2030 ambayo ni miaka michache tu ijayo tutakuwa ni bara la pili tumezidiwa na Asia, lakini tumewazidi Ulaya, Latini Amerika, Amerika ya Kaskazini kwa idadi ya watu wanaoishi mjini, kwa hiyo nayo ni changamoto kwa watengeneza sera.
"Lakini ni nafasi ya kiuchumi na kuchangamkia hii fursa kwa wawekezaji,washiriki au wadau wa sekta hiyo ndio kitu kikubwa nilitaka tuzungumze,"amesema Bw.Mchechu.
Nyumba watakazojenga
"Kwanza tunaangazia suala la kutawanyika mji unakwenda mbali zaidi, lakini pili tuna-focus kwenye vertical expansion kwa hiyo katika hili, ingawa kulikuwa na ujenzi mwingi unafanyika kulikuwepo nyumba za ubia wa maghorofa yamejengwa, lakini tumesema wakati huu twende tukalenge watu wa kundi la affordable housing ambazo tunakwenda kuzianzisha katika eneo la Kawe, Tanganyika Parkers.
Mkutano ukiendelea katika Ukumbi wa Kisenga Millenium Towers.
"Baadaye tutarudi mjini kwenye eneo la viwanja hivi ambavyo tunasema viko wazi na ndio maana kuna sababu ya msingi tunakwenda kufanya ujenzi huo.
"Pale Kawe tunaenda kuanza mwezi huu (Septemba) tunaenda kufanya pilot project, mwezi huu tunafikiria tuwe tumeanza foundation tutakwenda kujenga maghorofa 10 lile eneo zima la Kawe lina zaidi ya hakari 260 ambapo hekari 40 tulizitenga kwa ajili ya affordable apartment tu.
"Tunakwenda kutengeneza Apartment 'mablock' 10 kila moja litakuwa na apartment 40 kwa hiyo ndani ya kipindi hiki tunakwenda kufanya testing ya marketing kwa kutengeneza apartment 400.
"Sasa tukishaona hii concerpt ambayo tunaiweka ambayo tunakwenda kuwashirikisheni na nyie, ninaamini tutakwenda vizuri. Then tunakwenda kwenye measure scheme ambayo tunazungumzia apartment 5000. Lakini tunakwenda sehemu mbalimbali za nchi na tunafocus zaidi maeneo ya katikati ya miji.
"Blocks zina two wings na kila flool ina apartment nne nne huu mfumo nieleze tumeufikiria vipi? Katika kutengeneza huu mfumo tumeangalia vitu vingi kwanza kabisa uchumi halisi wa watu wetu, pili mtu anaweza asiwe anaishi pale, lakini anatumia nyumba yake very economical aweze kuishi nyumba na aweze kupata kipato chake.
"Hii nyumba ina three bedrooms ambapo moja ni studio, ina mlango wake mmoja wa kutoka moja kwa moja na pia mlango mwingine unaingia sitting room na jikoni ambazo hizi two bedrooms moja ni self contained na hii studio nayo ni self contained.
"Lakini kwa mtu ambaye yupo maisha ya kati au anaanza maisha ana uwezo wa kuishi kwenye vyumba viwili na kimoja akaweka mpangaji akapata fedha. Watoto kama hawapo nyumbani au wako masomoni kwa maeneo ya Kawe.
"Oviously kwa compaund ya high land Kawe unaitazama kwa sababu Kawe unaitazama na Mikocheni B, Mbezi Beach nayo rent yake iko resonable juu kwa sasa, lakini pia unaweza ukaamua ukae kwenye studio room hizi mbili ukaweka mpangisha. Hivyo ndivyo tulivyofikiria.
"Baada ya hizi pilot project kufanikisha hizi nyumba tutajitahidi kwenda kuzijenga sehemu mbalimbali hapa Tanzania. Lakini tutakachokuwa tunakifanya extarnal layout tutakuwa tunazitofautisha.
"Ndani tunaacha standard vile vile katika hizi block 10, block 7 tutawauzia wale wateja wenye uwezo wa kununua full apartment kwa maana ya vyumba vitatu ambacho ni two bedrooms na studio yako and then block tatu tutaziuza kwenye mchanganyiko.
"Kama kuna mtu mwenye uwezo wa kununua bedroom zake tutamwambia ruksa, nunua na kuna mtu mwenye kununua studio bedroom tunamwambia ruksa nunua.
"Tunataka walau three bedrooms iende kwa shilingi milioni 150 and two bedrooms could be around milioni 97 hadi 100 na quality hiyo na hiyo studio inaweza kuwa na milioni 46 inaweza kuja hadi milioni 50 may be after the accomplishment, hizo ndizo bei ambazo sisi tuna zi intend acutally price inaweza ikabadilika wakati wa ujenzi, lakini the main intent hatutaki kubadili.
"Hatutaki hizi nyumba zije zizidi shilingi milioni 200, hiyo milioni 150 ndiyo target yetu 160, 170, inategemeana saiti mambo yatakavyokuwa, hii ndio affordability tunaenda kuitekeleza. kwamba mtu mwenye milioni 50 atapata, mwenye 100 mwenye 150 atapata. Na niseme hii sio concerpt mpya sana niseme ni concerpt ambayo hapa katikati tulienda tukajisahau kuitengeneza.
"Kwa wale ambao mnafahamu nyumba zetu za Ubungo pale kuna apartment ambazo vina square mita 33 zile square mita 33 najaribu kufikiri kwamba wakati ule kipindi hicho cha Nyerere (Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere) na NHC watu walizipokea ilikuwa wakitoka chuo kikuu wanazitumia.
"Zile studio watu waliishi muda mrefu mpaka na wengine walipata wajukuu kwa hiyo zile studio zilikuwepo. Tunachokosa ni mwendelezo...la pili hizi nyumba tunaanza na Kawe tunasema tunajenga baada ya hapa viwanja vyetu vya mjini tunakwenda kujenga iwe ni Upanga sehemu yoyote ambayo tunafikiria kuna replacement.
"Lengo ni kwamba tunajikuta kwamba kwa sasa tuna Watanzania wanakaa mjini wanafanya kazi Mjini wakae hapo hapo Mjini na wanatembea kwenda maofisini kwao.
"Hawa wa Kawe watajiona wako mbali na mjini kwa muda mfupi, lakini dhamira ya kujenga Kawe, na tutaizungumza muda wake ukiwa tayari, Kawe tumeitengeneza kama new CBD (real properties located in a Central Business District) ambapo itakuwa na maofisi na makazi ya kutosha na tunayapeleka juu zaidi."
"Kwa sababu, tunataka Kawe i-operate 24 hours na unapotaka CBD i-oparate 24 hours tunahitajika minimum number of population ambayo itasapoti economic activities za mahali pale na ndio maana tunaleta hizi affordable zinazokwenda hadi juu,"amefafanua Bw.Mchechu.
Watu wataishije
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumzia juu ya namna ambavyo watu wataishi katika nyumba hizo amesema, "Watu wataishije? Tunasheria tayari ambayo imefanyiwa kazi na ndani yake constitution na sisi pia tunawajibika tunaokuwa members wa hizo association kwa wale ambao hawawezi kufuata utaratibu wa namna ya kuishi na sheria inatoa treatment ya hao watu nini kifanyike.
"Hii scheme ikienda vizuri tutakuwa na scheme kubwa ambayo inaitwa SHS kwa maana ya Samia Housing Scheme itaenda kujengwa nchi nzima. Kama nilivyosema kikubwa sana kinachotofautisha ni ile extarnal layout, lakini concerpt na thinking ya ndani ni ile ile na nyumba hizi tunatarajia kujenga takribani 5000 katika target ya phase ya kwanza.'
"Nyumba hizi tunategemea asilimia 50 tutazijenga Dar es Salaam ambapo ni maghorofa 55 na asilimia 20 jijini Dodoma kwa mahitaji maalumu ya makao makuu ya nchi kwa mliofika mtagundua kabisa kuna crisis ya nyumba hizo.
"Zingine mikoa mbalimbali, lakini si kila mkoa tulioupa asilimia tano utapata asilimia tano na tulioupa asilimia moja utapata asilimia moja, hizi tutaona lakini itategemeana na spidi na mahitaji ya huo mkoa wenye wateja wengi tunaweza kujenga asilimia 10 au 20.
"Kikubwa tunajenga hizi nyumba lengo letu la kwanza ni kuuza, tukikosa pale ambapo hazijauzika tunapangisha...kwa Dar es Salaam tuseme pilot project tunafanya Dar es laam na Dodoma eneo la Medeli,"amesema Mchechu.
Uhaba wa nyumba
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumzia kuhusu uhaba wa nyumba nchini amesema, "Si kweli kwamba NHC itakwenda ku-resolve matatizo ya nyumba kwa asilimia 100 hapa Tanzania.
"Lakini sisi tukichukua risk tukaanza private sector nao wanaweza wakafuatia kwa urahisi na pia tunakwenda kushirikiana nao, wana uwezo wa kuuza wao au tunashirikiana.
"Scheme hii ni kubwa inaenda kugenerate ajira zaidi ya 26000 na kuleta kodi mbalimbali tunakadiria mpaka concerpt nzima inakwenda kuisha phase one tutakuwa na VAT ya Bil.60, cooporate tax NHC Suppliers,benki bilioni 77, properties tax 0.05, PAYE bilioni 18 Bil. Total bilioni 155 ambayo ukijumlisha na 178 profit ya NHC, Serikali itapata zaidi ya shilingi bilioni 300 katika hii scheme ambayo tunaenda kuitekeleza.
"Hoja ya pili NHC haiwezi kutatua tatizo hili peke yake, actually nchi hii hata ungekuwa na NHC nyingi ambazo ni efficient hauwezi kutatua tatizo la nyumba kwa Watanzania. Lakini tumekuwa tukipata challenge Mheshimiwa Rais (Samia Suluhu Hassan) amezungumza na kutoa maagizo kuona Serikali na taasisi zake zinaingia makubaliano ya public-private partnerships (PPPs), sisi NHC tunaona ni kama fursa kwetu ni nafasi ya kutanua mbawa zetu.
"Kwa hiyo, tunaenda kufanya review ya policy mbalimbali tulizonazo na tulianza joint venture ya mwaka 1993, revise ya 1995, ya 2006 na revise ya 2012 na tunaifanyia revise tena sasa hivi, tunaenda kutengeneza product kama nne ambapo kutakuwa na kongamano rasmi na viongozi wetu. Tutaita wawekezaji ambao wako interested kuwekeza na NHC.
"Katika product tulizonazo ya kwanza ni Land as Equity Contribution (LEC) sisi NHC mchango wetu ni ardhi pekee, lakini zao hili tumetengeneza mazao mawili, wale watu wanatamani wawe na milki kubwa mwisho na wale wanaotamani kutengeneza faida.
Washiriki katika mkutano huo.
"Anayetengeneza faida atakuwa na ubia na sisi NHC kwa miaka 25 na baada ya miaka 25 sisi NHC tutabaki na asilimia 75 yeye 25 tunapoanza tunaanza na asilimia 25 to 75 na hii inakuja kwenye faida tunayotengeneza.
"Sisi tunachukua apartment zetu kadhaa na yeye tunamwachia asilimia 75 baada ya miaka 10 NHC tunaongeza asilimia 25 yeye anapunguza 25 percent tunakuwa tuko 50 kwa 50, baada ya miaka 10 tena tunachukua another asilimia 25 yeye asilimia 75 maana yake two at three end ya miaka 25 sisi tunachukua asilimia 75 yeye anabaki na asilimia 25 lakini kikubwa atakuwa anapata faida ya kutosha kabla hajafikia mahali hapo.
"Sasa tumepiga mahesabu hadi tunapokuja na hizi numbers na tumeangalia experience ya nyumba zetu tunapokuwa tunazicharge ni kutegemeana na maeneo na maeneo.
"Maeneo yenye high ritani actually unarahisisha wawekezaji wako 100 percent kwenye mwaka wa 9-11 hasa Kariakoo na Kariakoo unatengeneza hela yako ya pili, yale maduka ni vidogo lakini angalia kodi zinazochangiwa convert katika dola, Kariakoo square mita moja ni dola 60, lakini pana faida na watu wananunua kwa ajili ya biashara au kupanga kwa ajili ya biashara hii inamgusa mtu ambaye amekuja kwa ajili ya biashara na kuwekeza," amefafanua Bw.Mchechu.