“He is one of the greatest persons I have ever known, and I pray for the peace of his departed soul. Zacharia, you touched countless lives in your life time, and even ONE YEAR after your death, you live through your good deeds. We miss you always. Rest In Peace Zachari.” Magori
Huyu ni nani?
Zacharia Hans Poppe, ambaye alizaliwa mwaka 1956 jijini Dar es Salaam na kukulia mkoani Iringa, alifariki Septemba 10, 2022 majira ya jioni ambapo taarifa za kifo chake zilisambaa na kuhitimisha safari ya mwanamichezo, shabiki na mwanachama mtiifu wa Simba Sports Club.
Mpaka umauti unamkuta katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam, Zacharia Hans Pope alikuwa ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC.
Baba yake alikuwa ni raia wa Ujerumani na mama yake ni Mhehe wa Ipogoro lringa. Baba yake, Mzee Hans Poppe, alikuwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (RPC) wa Mkoa wa Ziwa Magharibi (sasa Kagera). Aliuawa na majeshi ya Idi Amin 1971, Mtukula, Kagera.
Baada ya kumaliza elimu ya Sekondari, Zacharia alijiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambako alifikia cheo cha Kapteni, kabla ya kuachishwa kazi na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela, kwa tuhuma za uhaini, dhidi ya Serikali ya Awamu ya Kwanza ya hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwaka
Lakini mwaka 1995, Zacharia aliachiwa huru kwa msamaha wa Rais wa awamu ya pili, Alhaj Ally Hassan Mwinyi, mwezi mmoja kabla hajamuachia Ikulu ya Tanzania, Benjamin William Mkapa, Rais wa awamu ya tatu ambaye kwa sasa ni marehemu.
Kama zinavyosema sheria za nchi, mtu aliyehukumiwa kifungo, hana haki ya kugombea wadhifa wowote au kuajiriwa tena, Zacharia naye hakuweza kurejea kazini, badala yake akaamua kujiajiri, kwa kuanzisha miradi yake mwenyewe, ikiwemo kampuni ya usafirishaji ZH Poppe.
Alianza kuipenda Simba SC mwanzoni kabisa mwa miaka ya 1970, akiwa kijana mdogo na zaidi mwenyewe aaliwahi kusema, mechi ambayo ilimfanya ajitamke rasmi yeye ni Simba damu ilikuwa dhidi ya wapinzani wa jadi, Yanga Juni 23, mwaka 1973, ambayo Wekundu wa Msimbazi, walishinda 1-0, bao pekee la Haidari Abeid (Muchacho) dakika ya 68.