NA DIRAMAKINI
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) imekutana chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa White House Makao Makuu jijini Dodoma tarehe 27 Septemba, 2022.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi,Shaka Hamdu Shaka.
Ameeleza kuwa, pamoja na mambo mengine Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imefanya uteuzi wa majina ya wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa CCM Wilaya kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2022 Ibara ya 82 (1) ambapo mikutano mikuu ya wilaya itafanyika kote nchini kuanzia Oktoba Mosi hadi 2, 2022.
Kwa mujibu wa tarifa hiyo, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC imeongeza muda wa kuchukua na kurejesha fomu kwa nafasi zote za Halmashauri Kuu Taifa ambapo zoezi hilo la kuchukua na kurejesha fomu litaanza Oktoba Mosi hadi Oktoba 5, 2022 kwenye ofisi za mkoa, Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar, Ofisi Ndogo ya Makamo Makuu jijini Dar es Salaam na Makamo Makuu ya CCM Dodoma.Yafuatayoi ni majina;