Rais Dkt.Mwinyi ateua viongozi mbalimbali leo

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Septemba 23, 2022 ameteua viongozi sita katika Wizara ya Afya.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said.

Mosi, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Dkt.Salim Nassor Slim kuwa Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya. Kabla ya uteuzi ho wa Dkt.Salim alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya.

Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua, Dkt.Msafiri Ladislaus Marijani kuwa Mkurugenzi Idara ta Tiba. Kabla, ya uteuzi huo, Dkt.Msafiri alikuwa Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Mnazi Mmoja.

Tatu, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Dkt.Fatma Mohamed Kabole kuwa Naibu Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya. Kabla ya uteuzi huo, Dkt.Fatma alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Maradhi Yasiyopewa Kipaumbele.

Nne, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua,Dkt.Muhidin Abdi Mahmound kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja. Kabla ya uteuzi huo, Dkt.Muhidin alikuwa Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Tano, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Khamis Bilal Ali kuwa Afisa Mdhamini Wizara ya Afya-Pemba. Kabla ya uteuzi huo, Khamis alikuwa Mkuu wa Idara ya Kinga na Elimu ya Afya-Pemba.

Sita, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Dkt.Farid Mzee Mpatani kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi ho, Dkt.Fariv alikuwa Afisa Mkuu Uchunguzi wa Maabara katika Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Zanzibar.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huu ambao umefanya na Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi kwa viongozi hao unaanza leo Septemba 23, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news