MAKAMU Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania (APNAC), Mhe. Cecilia Pareso (Mb) amesema mtandao wao utashirikiana kikamilifu na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa kwani rushwa inakwamisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Mhe.
Pareso amesema hayo jijini Dodoma wakati wa semina ya kuwajengea uwezo
wajumbe wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la
Tanzania (APNAC) ili waweze kushirikiana vema na TAKUKURU katika
kuitokomeza rushwa nchini.
“Sisi
wabunge ambao ni wajumbe wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa
Afrika tawi la Tanzania kwa pamoja tunaunga mkono juhudi za serikali
kuhakikisha rushwa inatokomezwa nchini kwa sababu kukiwa na rushwa
wananchi hawawezi kupata huduma wanayostahili,” Mhe. Pareso amesisitiza.