Serikali yatangaza msamaha kwa yeyote akayesalimisha silaha

NA DIRAMAKINI

SERIKALI ya Tanzania imetangaza msamaha wa kutokushitakiwa kwa mtu yeyote ambaye atasalimisha silaha anayoimiliki isivyohalali na kwamba usalimishaji huo utafanyika katika vituo vya Polisi, ofisi za serikali za mitaa au vijiji.

Pia mtu yeyote atakayepatikana na silaha haramu baada ya muda huo wa msamaha kupita atachukuliwa hatua kama mhalifu mwingine.
Akizungumza jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mwezi wa msamaha wa usalimishaji silaha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini amesema kuwa, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wataendesha kampeni maalum ambayo itashirikisha kamati za usalama za mikoa na wilaya, taasisi za kidini, vyombo vya habari na wadau wengine.
Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IJP Camillus Wambura amesema kuwa, hakuna mtu yeyote atakayechukuliwa hatua za kisheria atakaposalimisha silaha kwa hiari katika kipindi kilichotolewa kuanzia tarehe 01 Septemba 2022 hadi 31 Oktoba 2022 na kwamba mtu atakayepatikana na silaha anayoimiliki kwa njia ya haramu baada ya muda huo atachukuliwa hatua za kisheria.

IJP Wambura amewataka pia wanaomiliki silaha kihalali kuzingatia sheria na kanuni zilizopo ili silaha hizo zisiangukie kwenye mikono ya wahalifu

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news