NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa leo tarehe 27 Septemba, 2022 amefungua rasmi mabweni mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa shule ya Sekondari ya Kainam ya Mbulu mkoani Manyara.

Awali akizungumza kuhusu
mradi huo, Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kainam, Bw. Atnasi
Massay amesema mradi huo umesaidia wanafunzi kufanya vizuri kwani
umewaepusha na vishawishi kwa kuishi katika mazingira ya utulivu.

Kwa upande wake Meneja Miradi wa TEA, Masozi Nyirenda amesema TEA kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa imetumia kiasi cha Sh. Bilioni 1.39 katika miradi mbali mbali katika mkoa wa Manyara katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2015/2016 - 2019/2020.