NA DIRAMAKINI
LEO Septemba 29, 2022 wakazi wa Kijiji cha Nyamakobiti kilichopo Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wametuma salamu za pongezi na asante kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IJP Camillius Wambura na jeshi lote la Polisi kwa operesheni mbalimbali za kutokomeza wahalifu kijijini hapo na maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, wahanga wa vitendo vya uhalifu katika kijiji hicho wametoa
shuhuda mbalimbali kueleza namna walivyoteswa na matukio ya ujambazi kwa
kuibiwa mali zao kama vile mifugo, pikipiki pamoja na kujeruhiwa na
kuuliwa na majambazi sugu kijijini hapo kabla ya Jeshi la Polisi
kuwashugulikia kikamilifu.