NA TITO MSELEM-WM
KATIBU Mkuu Wizara ya Madini Adolf Ndunguru ametoa wito kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini kushiriki Maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini 2022 mkoani Geita kwa lengo la kujifunza namna bora ya utendaji wa shughuli zao.

"Wizara ya Madini inayo mikakati mbalimbali ya kuwasaidia wachimbaji wadogo ili waweze kupata elimu ya uchimbaji madini na hatimaye waweze kuchimba kwa tija," amesema Ndunguru.


"Nimepata taarifa kwamba, zaidi ya kampuni na taasisi 800 zimealikwa kushiriki katika maonesho haya lakini kampuni 602 ndiyo zimethibitisha kushiriki hivyo, niuombe mkoa wa Geita na waandaaji wote kwa ujumla kuendelea kuyatangaza maonesho haya ili wadau wa madini wa ndani na nje ya nchi waweze kushiriki kwa wingi zaidi," amesema Mbibo.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Ndunguru ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Mbibo, Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrahman Mwanga na Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba.