NA DIRAMAKINI
LEO Septemba 22, 2022 wadau mbalimbali wameshiriki katika mjadala maalum na muhimu wa Kitaifa ukiangazia juu ya punguzo la tozo na faida zake kwa wananchi.


WILLIAM MHOJA, KAMISHINA MSAIDIZI IDARA YA SERA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

"Kama tutaamua kuzifuta kabisa hizi tozo basi tutachelewa na kurudi nyuma katika kuhakikisha tunatanua wigo wa maendeleo kwa shughuli zile ambazo tumezikusudia na kuikwamua nchi,"amesema.
DKT.ABDALLAH S. MABODI, NAIBU KATIBU MKUU CCM ZANZIBAR
"Mawazo ya waziri yalikuwa mazuri sana kwamba hizi fedha za tozo zitakazo kusanywa zitakwenda kutoa mahitaji ya msingi ya kimaendeleo kwa watu wa hali ya chini, ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya, shule, nyumba za walimu, upatikanaji wa vitendea kazi mashuleni na hospitalini n.k.



DKT.HEZRON MAKUNDI, MTAFITI TAALAM ZA MAENDELEO ( USDM)
"Sehemu kubwa ya wajibu wa serikali ni pamoja na kusimamia masuala ya fedha, kwani ina nafasi kubwa sana katika uendeshaji wa dola au Taifa, hii ni pamoja usimamizi wa mapato ya ndani kuhakikisha yanasaidia taifa kusonga mbele.


MHE. GOODLUCK NG'INGO, MWANADIPLOMASIA NA MCHAMBUZI MASUALA YA KISIASA
"Sote tunakiliri kwamba Serikali Awamu ya Tano na Sita chini ya Mhe.Rais Samia kupitia fedha za makusanyo imetekeleza miradi mingi sana kwa kipindi kifupi kila mtanzania anajua hilo siyo mijini bali asilimia kubwa miradi hiyo ipo vijijini kwa wahitaji zaidi.


AZIM DEWJI, MFANYABIASHARA
"Kwa sisi wafanyabiashara ongezeko hili la tozo lilikuwa linatupa wakati mgumu hasa kwenye ushindani masokoni, kwa sababu tozo ikiongezeka hasa kwenye mazao bei lazima iwe juu, hii inatufanya wale washindani wetu hasa nje ya nchi wanatuzidi kwa sababu bei yetu ipo juu.