Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita, Mhe. Jamhuri David William (kulia) akipewa maelezo na Afisa kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa, Bw. Edgar Mwakasitu, kuhusu namna Benki Kuu ya Tanzania inasimamia mifumo ya malipo ya taifa nchini alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Tano ya Biashara ya Madini yanayofanyika kitaifa mkoani Geita.
Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita, Mhe. Jamhuri David William, akielezea jambo alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Tano ya Biashara ya Madini yanayofanyika kitaifa mkoani Geita.


Afisa kutoka Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Bi. Rukia Muhaji, akifafanua jambo kuhusu namna DIB inakinga amana za wateja wa mabenki nchini kwa Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita, Mhe. Jamhuri David William (kulia) alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Tano ya Biashara ya Madini yanayofanyika kitaifa mkoani Geita.(Picha na Benki Kuu).