Waziri Balozi Dkt.Chana afanya uteuzi Bodi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi H. Chana (Mb), kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 5(1) na 5(4) cha Sheria ya Wakala za Serikali Sura ya 245, amemteua Brigedia Jenerali Mbaraka Naziad Mkeremy kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
Aidha,Mheshimiwa Waziri Balozi Dkt.Pindi Chana amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa hiyo:-

1. Dkt. Siima Salome Bakengesa, Mkurugenzi wa Utafiti na Uzalishaji wa Misitu, Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI).

2. Eng. Enock Nyanda Emmanuel, Mkurugenzi Msaidizi – Uchumi na Uzalishaji, Ofisi ya Rais TAMISEMI.

3. Adv. Piensia Christopher Kiure, Mkurugenzi wa Uhusiano, Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).

4. CPA. Bahati Lucas Masila, Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais.

Aidha, kwa mujibu wa Kifungu cha 5(5) cha Sheria ya Wakala za Serikali Sura 245, Prof. Dos Santos Aristariki Silayo, Kamishna wa Uhifadhi - TFS, anakuwa Katibu wa Bodi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Maliasili na Utalii, uteuzi huu ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 23 Septemba, 2022 hadi 22 Septemba, 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news