Waziri Balozi Mulamula ashiriki Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa UN wa Usuluhishi

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula ameshiriki Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi unaofanyika sambamba na Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula akishiriki Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi unaofanyika sambamba na Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula akijadiliana jambo na washiriki wa Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi uliofanyika jijini New York.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula akiwa katika Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi ujijini New York.
Wenyeviti wenza wa Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi Uturuki na Finland wakiwasikiliza washiriki wa kikao hicho.

Akizungumza katika mkutano huo Balozi Mulamula amesema usuluhishi ni njia muhimu katika kutatua changamoto za migogoro duniani na kuusihi Umoja wa Mataifa kuliingiza suala la usuluhishi katika mifumo ya utatuzi wa migogoro ya Umoja wa Mataifa.

Amesema usluhishi ukiingizwa katika mifumo ya utatuzi ya migogoro ya Umoja huo utasaidia shughuli za upatanishi na utatuzio wa migogoro na hivyo kuufanya Umoja huo kufikia lengo la utatuzi wa migogoro na kuifanya dunia kuwa sehemu salama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news