NA DIRAMAKINI
WAZIRI wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe.Dkt.Ashatu Kijaji amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini (Blueprint) ili kuvutia uwekezaji na kuwezesha ufanyaji biashara wenye tija utaokuza uchumi wa taifa kwa ujumla.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma leo Septemba 29, 2022.
Akiwa ameambata na viongozi wa Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara akiwemo Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Hashil Abdallah, Dkt. Kijaji amemhakikishia Mkurugenzi huyo kuwa Serikali iko tayari kushirikiana na Benki ya Dunia kuanzisha na kuendeleza programu mbalimbali za kuwawezesha wajasikiamaki wadogo na wa kati kuwekeza na kufanya biashara ili kukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.
Aidha, Dkt. Kijaji amesema Serikali inaendelea kufanya mamoresho mbalimbali kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini ( Blueprint) ikiwemo kupitia na kurekebisha sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Uwekezaji pamoja na kupunguza tozo mbalimba ambazo zimekuwa kikwazo katika ufanyaji biashara na uwekezaji.