NA GODFREY NNKO
WAZIRI wa Utumaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (Mb),amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kukutana mara moja na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) ili kutathmini mwenendo wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) na kuandaa mkakati wa pamoja wa kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri na kupata mafanikio yanayotarajiwa.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 6, 2022 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw.John Mapepele.
Agizo hili limetokana na mwenendo usioridhisha wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya (Taifa Stars) ambayo imekuwa ikishiriki mashindano ya Kimataifa mara kwa mara bila kufanya vizuri sana ikilinganishwa na timu nyingine za Taifa ikiwemo timu za Taifa za Mpira wa Miguu kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Mhe. Mchengerwa ameagiza kikao hicho maalum kifanyike mara moja na apokee taarifa ya utekelezaji wa maelekezo haya ndani ya siku 14 tangu tarehe ya leo.
Wakati huo huo, Waziri Mchengerwa amelielekeza BMT kufuatilia tukio la pambano la ngumi la Bondia wa Tanzania Hassan Mwakinyo lililofanyika nchini Uingereza dhidi ya Bondia Liam Smith.
Ieleweke kuwa Serikali haipo tayari kuona mazingira yeyote ya sintofahamu kwa wachezaji wa kitanzania wanaposhiriki mashindano hasa ya kimataifa.
Aidha, ameelekeza kufanyika kwa mabadiliko ya watendaji kwenye Kurugenzi ya michezo ili kupata watu wenye sifa na kiu ya mafanikio, weledi, wachapakazi na wabunifu ili kuleta maadiliko ya kweli kwenye sekta ya michezo.