NA MATHIAS CANAL-WEST
SERIKALI imekanusha taarifa za uzushi zilizotolewa kuhusu tarehe ya shule kufunguliwa iliyotolewa na baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema na sekta ya elimu nchini.
Taarifa hiyo imeenea katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikieleza kuwa shule zitafunguliwa tarehe 21 Septemba 2022 jambo ambalo sio sahihi na hakuna muongozo wala maelekezo hayo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amekanusha uvumi huo leo Septemba 3, 2022 wakati akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Skuli ya Ole Sekondari iliyopo katika Mkoa wa Kusini Pemba jijini Zanzibar wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja visiwani humo.

“Naomba mpuuze jambo hili kwanza aliyesambaza anatumia nembo ya kampuni moja ambayo kampuni hiyo haijui na haihusiki na tangazo hilo, kwa hiyo hakuna maelekezo yoyote zaidi ya yale yaliyotolewa na Kamishna wa Elimu,"amemesema Waziri Mkenda.
Kuhusu mageuzi ya elimu, Waziri Mkenda amesema kuwa serikali inafanya mapitio ya sera ya elimu ya mwaka 2014 pamoja na mapitio ya mitaala ili kuboresha sekta ya elimu.

