NA MATHIAS CANAL-WEST
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Prof. Adolf Mkenda (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania, Mhe Alvandi Hossein pamoja na Rais wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa (Al-Mustafa International University) cha nchini Iran, Dkt Ali Abbasi.
Katika mazungumzo hayo Waziri Mkenda na wageni hao kutoka Iran, wamekubaliana kuendeleza ushirikiano kwenye taasisi za elimu ya juu katika masuala ya Teknolojia, Sayansi, na Elimu ujuzi.
Waziri Mkenda amemuomba Balozi huyo kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kubadilishana utaalamu baina ya Vyuo Vikuu vya hapa nchini na Iran ili kuongeza wigo wa ujuzi kwa pande zote mbili.