Waziri Prof.Mkenda:Serikali imetenga Bilioni 100/- ujenzi vyuo vya VETA nchini

NA MATHIAS CANAL-WEST

SERIKALI inayo azma ya kujenga Chuo cha Ufundi Stadi katika kila Mkoa na Wilaya nchini ambapo katika mwaka huu wa fedha 2022/2023 imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 100 kutekeleza mpango huo.
Kiasi hicho cha fedha ni kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi katika Wilaya 62 kwa Wilaya ambazo zilikuwa hazijajengewa Vyuo vya Ufundi Stadi.

Aidha, Wilaya ya Manyoni ni miongoni mwa wilaya hizo 62 ambazo zipo kwenye mpango wa kujengewa Vyuo vya Ufundi Stadi kwa mwaka huu wa fedha.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda amesema hayo leo Septemba 21,2022 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe Dkt. Pius Stephen Chaya, Mbunge wa Jimbo Manyoni Mashariki aliyetaka kufahamu serikali ina Mpango gani wa kujenga Chuo cha VETA Wilayani Manyoni.

Waziri Mkenda amesema kuwa katika mwaka huu wa fedha 2022/23, Serikali imetenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi katika Wilaya 62 kwa Wilaya ambazo zilikuwa hazijajengewa Vyuo vya Ufundi Stadi.
Aidha, Prof Mkenda amesema kuwa Wilaya ya Manyoni ni miongoni mwa Wilaya hizo 62 ambazo zipo kwenye mpango wa kujengewa Vyuo vya Ufundi Stadi kwa mwaka huu wa fedha.
Waziri Mkenda amewashauri wananchi wa wilaya ya Manyoni wakiwemo wa Jimbo la Manyoni Mashariki waendelee kutumia Chuo cha Ufundi Stadi cha Mkoa wa Singida, na Chuo cha Wilaya ya Ikungi, Pamoja na Vyuo vya Singida na Msingi FDC na Vyuo vingine vya ufundi stadi vilivyopo nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news