Waziri Simbachawene akabidhiwa Jedwali la Uchambuzi wa Sheria Ndogo

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe.George Simbachawene amepokea Jedwali la Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Bunge wa Saba kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Ramadhani Suleiman.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe.George Simbachawene (kushoto) akipokea Jedwali la Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Saba wa Bunge

Akizungumza wakati wa kupokea Jedwali la Uchambuzi wa Sheria Ndogo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. George Simbachawene, Septemba 2, 2022 amesema, Serikali inaongozwa na sheria zinazotungwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe.George Simbachawene (katikati) akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, katika Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.

“Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo inaweza kutatua changamoto zote zinazogusa watu katika maswala ya sheria, kanuni, taratibu, mila na desturi zinazoongoza Serikali,"amesema Waziri Simbachawene.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo Mhe. Ramadhani Suleiman (katikati) akifafanua jambo.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo Mhe. Ramadhani Suleiman amemshukuru Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu kwa kupokea Jedwali la Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Saba pamoja na majibu aliyoyatoa kwa Kamati ya Bunge.
Mhe. Judith Kapinga akifafanua jambo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo ilipokabidhi Jedwali la Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Saba wa Bunge kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu.(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news