Wizara ya Ardhi: Ukiombwa malipo kinyume na utaratibu uliowekwa toa taarifa 0739646885

NA GODFREY NNKO

WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa maelekezo kuhusu gharama za utoaji huduma katika ofisi za ardhi kote nchini ambapo imewataka wananchi watakaoombwa malipo kinyume na utaratibu uliowekwa kisheria kutoa taarifa.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Septemba 12, 2022 na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

"Wizara imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu kutozwa gharama kinyume na sheria na kanuni ambazo zimeainisha ada na tozo mbalimbali kwa ajili ya upatikana wa huduma za ardhi.

"Huduma hizo ni pamoja na zinazohusiana na kwenda uwandani kuonyeshwa viwanja, kutatua migogoro,kuchukua taarifa kwa ajili ya uthamini n.k.

Kufuatia malalamiko hayo, Katibu Mkuu Dkt.Allan Kijazi amewatangazia wananchi wote kuwa ada na tozo kwa ajili ya huduma za ardhi zimeanishwa kwenye sheria, kanuni na miongozo inayosimamia utoaji wa huduma za Sekta ya Ardhi.

"Huduma zinazohitaji malipo hufanyika kwa kuzingatia taratibu za malipo ya Serikali ikiwa ni pamoja na kupata namba ya kumbukumbu ya malipo (control number) na stakabadhi ya malipo. Wananchi watakaoombwa malipo kinyume na utaratibu uliowekwa kisheria, mnaombwa kutoa taarifa kwa uongozi wa ofisi za Halmashauri, Ardhi Mikoa, au Makao Makuu ya Wizara, au kupitia namba 0739646885,"imefafanua sehemu ya taaarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news