Balozi Chipeta awasilisha hati za utambulisho kwa Mfalme wa Uholanzi

NA MWANDISHI WETU

BALOZI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Falme ya Uholanzi , Mhe. Caroline Kitana Chipeta, awasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Mfalme Willem-Alexander wa Uholanzi.
Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Caroline Kitana Chipeta akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Mfalme Willem-Alexander wa Uholanzi.
Balozi wa Tanzania katika Falme ya Uholanzi, Mhe. Caroline Kitana Chipeta akizungumza na Mtukufu Mfalme Willem-Alexander wa Uholanzi baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.
Balozi wa Tanzania katika Falme ya Uholanzi, Mhe. Caroline Kitana Chipeta katika picha na Mtukufu Mfalme Willem-Alexander wa Uholanzi baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mfalme huyo.
Balozi wa Tanzania katika Falme ya Uholanzi, Mhe. Caroline Kitana Chipeta katika picha ya pamoja na maafisa Ubalozi wa Tanzania nchini humo baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mfalme wa Uholanzi.
Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Caroline Kitana Chipeta alipowasili katika kasri lililoko Noordeinde, The Hague, Uholanzi kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Mfalme Willem-Alexander wa Uholanzi.

Hafla hiyo imefanyika katika moja ya Kasri za Kifalme iliyoko Noordeinde, The Hague, Uholanzi tarehe 19 Oktoba, 2022.

Julai 2022, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alimteua Balozi Caroline Kitana Chipeta kuwa Balozi wa Tanzania katika Falme ya Uholanzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news