Baraza la Wafanyakazi REA laaswa kuleta matokeo chanya

NA VERONICA SIMBA-REA

WAJUMBE wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wameaswa kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi ili kuleta matokeo chanya kwa Wakala.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Elineema Mkumbo, akifungua rasmi mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Baraza la Wafanyazi, Oktoba 11, 2022 jijini Arusha. Mafunzo hayo yanatolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
Wito huo umetolewa leo, Oktoba 11, 2022 jijini Arusha na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Elineema Mkumbo, wakati akifungua mafunzo rasmi ya kuwajengea uwezo Wajumbe hao, yanayotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu.
Mhandisi Mkumbo amewasisitiza Wajumbe wa Baraza kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo ya siku tatu ili yawawezeshe kusaidia Wakala katika kutekeleza kwa tija na kutimiza malengo ya kuhakikisha wananchi walioko vijijini wanapata nishati bora ili kuboresha maisha yao.

“Kila mmoja afuatilie mafunzo haya kwa umakini. Haifai kuona mtu amepata nafasi hii adhimu, halafu anaacha kuitendea haki Taasisi,” amesisitiza Mhandisi Mkumbo.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Aziz Abbu, akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Baraza hilo, Oktoba 11, 2022 jijini Arusha. Mafunzo hayo yanatolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Akizungumzia lengo la mafunzo hayo, Katibu wa Baraza la Wafanyakazi REA, Aziz Abbu, ameeleza kuwa ni kuwajengea uwezo Wajumbe wake kwa maana ni Baraza jipya lililoundwa mwezi Mei mwaka huu.

“Ni vema Wajumbe wajue wajibu na majukumu yao ili waweze kuiwakilisha vyema Taasisi,” ameeleza Aziz.
Afisa Elimu Kazi Mwandamizi, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Emiliana Rweyendela, akiendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Oktoba 11, 2022 jijini Arusha.

Kwa upande wake, Mwezeshaji wa Mafunzo hayo ambaye ni Afisa Elimu Kazi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Emiliana Rweyendela, amesema washiriki watapata uelewa wa dhana ya ushirikishwaji wafanyakazi mahala pa kazi ili kujua wajibu na haki zao.
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo yanayotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, jijini Arusha. Mafunzo hayo ya siku tatu yamefunguliwa rasmi leo, Oktoba 11, 2022.

Akifafanua zaidi, Rweyendela ameeleza kuwa shabaha ya ushirikishwaji inalenga kupunguza matumizi mabaya ya madaraka yanayotokana na utaratibu wa kubana njia za mawasiliano lakini pia kujenga jamii isiyokuwa na matabaka na kumwezesha mfanyakazi kushiriki katika kutunga será na mipango ya uchumi kitaifa.

Aidha, Rweyendela amesisitiza kuwa ushirikishwaji wa wafanyakazi nchini ni vyema ukatazamwa kwa mwelekeo wa kukuza tija na ufanisi sehemu za kazi jambo ambalo haliepukiki katika mifumo yote ya utendaji kazi.
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo yanayotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, jijini Arusha. Mafunzo hayo ya siku tatu yamefunguliwa rasmi leo, Oktoba 11, 2022.
“Katika wakati huu tulionao wa utendaji kazi ambao ni wa kuingia mikataba na waajiri na kuangalia ubora wa huduma kwa wateja na mfanyakazi kujitathmini mwenyewe, pamoja na mfumo wa upimaji kazi wa wazi, kuna haja kubwa ya kushirikishana shughuli zote za Taasisi ili kuwa na uelewa wa pamoja,”amesema.

Baraza la Wafanyakazi REA limeundwa kwa uwakilishi wa kila Kitengo, Idara pamoja na Menejimenti.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news