NA ROTARY HAULE
WAKALA ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umewataka wadau mbalimbali wa biashara na wawekezaji kusajili jina la biashara au kampuni zao mapema kabla hawajaanza kufanya biashara.

Mfinanga amesema kuwa, moja ya changamoto wanayokumbananayo wakati wa usajili ni pale ambapo mtu anasajili jina la biashara wakati tayari lina mtu anayelitumia.
Amesema kuwa,wafanyabiashara wengi wanaanza kufanya biashara zao halafu baadae wanakwenda kusajili jina jambo ambalo limekuwa likileta changamoto katika usajili kwani wanapotaka kusajili wanakuta tayari analotaka kusajili lilishasajili muda mrefu.

Mfinanga amesema kuwa, endapo watakuwa wamesajili mapema itasaidia kuondoa usumbufu na kuwapunguzia adha ya kutafuta majina mengine hali ambayo itakuwa inawapotezea muda.
Amesema kuwa,BRELA imeshiriki Maonesho ya Wiki ya Biashara na Uwekezaji mkoani Pwani kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara kupata leseni zao,kusajili majina ya biashara na kampuni kirahisi.

Amesema,kila mkoa wamekuwa wakishiriki maonesho hayo na kwa upande wa Mkoa wa Pwani mwaka huu ni mara ya tatu kushiriki na wapo tayari huku akisema mhitiko wa wadau,wafanyabiashara na wawekezaji ni mkubwa bandani hapo.
"Kwa kweli tunashukuru maana mwitiko wa watu hapa bandani kwetu ni mkubwa,wapo wanakuja kutaka leseni,majina ya kampuni na hata majina ya biashara,"amesema Mfinanga.
Hata hivyo,amewataka wanachi,wadau, wawekezaji na wafanyabiashara kutembelea banda hilo la BRELA ili kupata huduma kwa wakati na kwamba watakuwepo katika maonesho hayo mpaka Oktoba 10, mwaka huu.